Jumamosi, 21 Machi 2015

WATU 126 WAUAWA MISIKITINI YEMEN.

Zaidi ya watu 126 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa, baada ya watu wa kujitolea muhanga kujilipua misikitini nchini Yemen. Watu hao wameuwawa katika milipuko iliyolenga misikiti katika mji mkuu Sanaa wakati wa sala ya Ijumaa. Waandishi Habari wanasema kuwa, misikiti yote miwili ni maeneo ya maombi kwa waislamu wengi ambao aaasi wa Ki-Shia, maarufu kwa jina Houthis, wanaodhibiti mji mkuu wa Sanaa. Kwa miezi kadhaa sasa, kumeshuhudiwa taharuki kubwa kati ya makundi hasimu nchini Yemen, pamoja na makundi yaliyo na uaminifu na mtandao wa Al-Qaeda yaliyo katika maeneo ya kusini na mashariki mwa taifa hilo.

BBC.

Jumatano, 18 Machi 2015

MAKAMU WA RAIS WA SIERRA LEONE AFUTWA KAZI.

Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma amemfuta kazi makamu wa rais kwa kutafuta hifadhi katika ubalozi wa kigeni nchini humo. Siku ya jumamosi ,Samuel Sam Sumana amesema kuwa alimtaka balozi wa Marekani kumpatia hifadhi ndani ya ubalozi wa Marekani nchini humo akihofia maisha yake. Awali wanajeshi waliizunguka nyumbani yake na kumpokonya silaha mlinzi wake . Kumekuwa na wasiwasi kati ya rais na bwana Sam Sumana. Hivi majuzi aliondolewa katika chama tawala cha All People Congress kwa udanganyifu na kuchochea ghasia. Hatahivyo amekana madai hayo.

BBC.

AL SHABAAB:WATU 3 WAUAWA WAJIR,KENYA.

Maafisa wa polisi nchini Kenya wanasema kuwa takriban watu watatu wameuawa katika mji wa kazkazini wa Wajir, yapata kilomita 100 kutoka mpaka na Somalia. Watu waliofunika nyuso zao walishambulia duka moja na kufyatua risasi, kulirushia magurunedi kabla ya kulichoma. Kundi la wapiganaji wa Al-Shabaab limeongeza mashambulizi yake kazkazini mashariki mwa Kenya katika siku za hivi karibuni ,na kufanya mashambulizi mawili katika mji wa Mandera ambao una pakana na Somali. Kundi hilo linadhibiti eneo kubwa la Somalia la mashambani na limesajili idadi kubwa ya raia Wakenya.

BBC.

WATALII17 WA KIGENI WAUAWA TUNISIA.

Jengo la kumbukumbu la Tunisia lililolengwa na wapiganaji na kusababisha mauaji ya watu saba Watu 19 wakiwemo watalii 17 wa kigeni wameuawa baada ya wapiganaji kulenga jengo moja la kumbukumbu za kihistoria katika mji mkuu wa taifa hilo amesema.Rais wa Itali,Uhispania na Wajerumani ni miongoni mwa wale waliouawa waziri mkuu Habib Essid amesema. washambuliaji wawili pamoja na afisa mmoja wa polisi wameuawa katika oparesheni ya kiusalama iliofanywa,maafisa wanasema.Shambulio hilo lilifanyika katika jengo la kumbukumbu la Bardo Museum ambalo liko jirani na bunge katikati mwa Tunisia wakati wa shambulio hilo,wabunge walikuwa wakijadiliana kuhusu sheria dhidi ya ugaidi. Watu wameondolewa katika majengo ya bunge. Raia wa Uingereza,Italy,Ufaransa na Uhispania ni miongoni mwa waliotekwa wakati wa shambulizi hilo,kituo kimoja cha redio nchini humo kimetangaza. Mateka waliosalia katika jumba hilo la kumbukumbu wameachiliwa ,shirika la habari la Reuters limesema baada ya kupata habari hizo kutoka kwa afisa mmoja wa serikali ambaye hakutaka kutajwa.

BBC.

Jumapili, 15 Machi 2015

MILIPUKO YALENGA MAKANISA PAKISTAN.

Wasichana walia kufuatia mashambulizi mawili yaliolenga makanisa Pakistan Mabomu mawili yamelipuka yakilenga makanisa mawili yaliyokuwa yamejaa watu kwenye mji wa Lahore chini Pakistan wakati watu walipokuwa wakihudhuria misa ya jumapili. Polisi wanasema kuwa takriban watu 6 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Mashambulizi hayo yanaoyoaminika kuwa ya kujitoa mhanga yalifanyika eneo lenye waumini wengi wa kikristo la YouhanabadH Sehemu ya kundi la Taliban linalofahamika kama Jamatul Ahra limesema kuwa ndilo lililoendesha shambulizi hilo.

BBC.

Jumamosi, 14 Machi 2015

PAPAI.

Papai ni tunda la mmea unaofahamika kama "carica papaya" wa jenasi corica, unaasili ya amerika ya kaskazini na unakuwa huko maksiko, karne kadhaa kabala ya kuibuka kwa tamaduni mpya za huko amerika, Ni mti mkubwa wenye shina la urefu wa mita 5 mpaka 10, yenye majani yaliojipanga yaliojizungusha na kujishikiza juu kwenye shina la miti, shina kwa upande wa chini huwa na makovu mengi kuonesha sehemu ambayo majani yalikuwa majani ya mpapai ni makubwa sm 50 – 70 kwa upana, maua yake ni madogo na hutokea sehemu yalipochomoza majani, hutengeneza tunda papai lenye urefu wa sm 15- 45, na upana wa sm10 – 30. Tunda huiva pale linapokuwa laini ( kama vile parachichi au zaidi) na ngozi yake inapokuwa na ngozi yake inapo karibia rangi ya chungwa ladha ya chungwa hukamilana na ile kati ya nanasi na peasi, ingawa huwa ya utulivu bila ya uchungu wowote. [hariri]Wingi na matumizi ya papai Kutoka asili yake ya Meksiko, Puerto rico amerika ya kati na kusini mwa asia . Papai lililoiva huliwa bila ya maganda wala mbegu zake papai bichi huliwa baada ya kuchemshwa na kupimwa pamoja na saladi ya michemsho mingine. Papai bichi na mti wake huwa na utovu. Yenye kemikali inayoitwa ‘papari’ ambayo hutumika kulainisha nyama kwa kuvunjavunja protini iliyondani yake. Uwezo wake huu wa kulainisha nyama ngumu umetumiwa tangu enzi za zamani na watu wa kale. Wanawake huko india, Pakistani, sililanka walitumia sana papai kama njia ya kuzuia mimba na hata kutoa mimba wanawake waliokuwa utumwaniai pia walionekana sana wakitumia sana papai ili kuzuia wasishike mimba na kuwazaa watoto wao utumwani imegundulika hatambegu za papai nazo huweza kusababisha kuondoa uwezo wa kuzaa kwa wanaume. Shina na matawi ya mipapai pia yanatumika kutengenezea kamba. mbegu zaidi za mipapai huweza kuliwa na zina radha kali sana. Hu8sagwa na wakati mwingine na kutumiwa kama mbadala wa pilipili. Sehemu Fulani za asia, majani machanga ya mmea wa mpapai huchemshwa kwa mvuke na kuliwa kama spinachi. Sehemu Fulani duniani majani ya mpapai hunyweshwa na chai kama dawaya kutibu malaria, japo hakuna ushahidi wa kutosha juu ya matibabu haya. [hariri]Hatari ya matumizi ya papai na mazao yake Tunda la papai, mbegu na utomvu wake, pia majani yake yana kiwango kikubwa cha carpaine’ kemikali inayoondoa minyoo kwenye mwili lakini matumizi ya kiasi kikubwa huweza kuwa hatari. Inafahamika kuwa mapapai mabichi yanaweza kusababisha kutoka kwa mimba kutokana na kiwango kikubwa cha kemikali ya Latex ambayo husababisha kuta za uterasi kusinyaa japo haijathibitishwa bado. Kula sana mapapai kama ilivyo kwa karoti, huweza kusababisha ugonjwa wa karotinemia ambapo nyayo na viganja huwa vya rangi ya njano japo hakuna madhara yoyote. Mbegu za Matikiti maji faida yake ni hii: chukua mbegu za tikiti maji zikaange halafu zitwange ili zitoe unga, chukua juici ya kitunguu thaumu lita moja na asali lita moja changanya pamoja juisi ya kitunguu thaumu na asali weka na vijiko kumi vikubwa vya unga wa tikiti maji koroga vizuri na uwe unakunya dawa hii kikombe kimoja cha kahawa mara tatu kila siku kwa muda wa wiki moja. Jamani Mlonge ni dawa na tiba kubwa sana Nimesikia mengi kuhusiana na mti wa Mlonge lakini hii ni kali zaidi CAPE TOWN, (IPS). Wakati tatizo linalipolikabili Bara la Afrika, watu wanaangalia uwezekano wa kupata misaada kutoka kwenye mashirika ya kimataifa kutoka nje ya bara hilo. Lakini hali ya ukame inayoongezeka kwa kasi, miti yenye kuhimili ukame huku ikiwa na majani yenye viini lishe vingi inaweza kuwasaidia watu maskini, pia maeneo ya usalama wa chakula na utapiamlo, wao wenyewe. Shamba lenye hekta 15 lilipandwa miti ya Mlonge au wengine huuita mti wa miujiza ambao kwa Kiingereza unaitwa Moringa Oleifera, tayari umeshaanza kuleta mabadiliko katika jimbo moja maskini zaidi la Afrika Kusini la Limpopo. Majani ya Mlonge yamepachikwa jina la chakula chenye viwango kwasababu wanasayansi waligundua yana kiasi cha madini ya Kalisium yanayoweza kupatiakana katika glasi nne za maziwa, kiasi cha vitamini c inayopatikana kwenye machungwa saba, Potasium ya kwenye ndizi mbivu tatu. Pia unapata kiasi cha madini ya chuma mara nne zaidi ya kiasi kile kinachopatikana kwenye spinachi. kiasi cha vitamani A mara nne zaidi ya kile kinachopatikana kwenye karoti na kiasi cha protini mara mbili zaidi ya kile kinachopatikana kwenye maziwa. Ukiwa na mti wa Mlonge ni sawa na kuwa na Supermarket kwenye mti. Mavis Mathabatha aliyewahi kuwa mwalimu kutoka Tooseng, amekuwa akifanya bidii ya kufungua mashamba ya Mlonge kwa kipindi cha miaka mitatu sasa ambalo litamuwezesha kuzalisha majani ya kutosha ya Mlonge ili kusaidia kuleta mabadiliko katika jamii yake. "Nataka kuleta mabadiliko katika jimbo langu na nchi nzima kupitia mradi huu," alisema. Mwaka 2009, alianza kuvuna na kuyakausha na kisha kuyasaga majini ya Mlonge kutoka kwenye miti michache aliyokuwa ameipabnda. Unga huo wa Mlonge alikuwa ukiwachanganyia watoto 400 kutoka katika familia masikini waliokuwa wakipata chakula kutoka kwenye kituo maalum. Kituo hicho kinalisha watoto wanaotoka katika familia zenye kipato kidogo ambacho kiko chini ya dola 250 kwa mwezi. Hii inahusuisha watoto wote wa kike na kiume kutoka kwenye jamii hiyo ambayo ina tatizo la ukosefu wa ajira, umasikini na utapiamlo, wengine wana maambukizi ya UKIMWI. "Matokeo yake yalikuwa dhahiri kwa muda mfupi sana, Afya za watoto ziliboreka kwa muda mfupi. Anasema Elizabeth Serogole, meneja wa kituo hicho cha kulisha watoto ambaye anafanya kazi kwa kushirikiana na Mathabatha. Anasema watoto wengi waliokuwa wakionesha kuwa na utapiamlo, kama vile vidonda kwenye ngozi walianza kupona mara baada ya kula mlo huo uliochanganywa na unga wa Mlonge. Nyongeza hiyo ya Mlonge kwenye chakula chao iliwasaidia kupambana na magonjwa mengine yaliyojitokeza, pia iliwasaidia kuboresha uwezo wao wa kiakili," anasema Seregole. "Wengi sasa wanaweza kusoma vizuri shuleni," anasema. Walichokuwa wanahitaji ni kjiko kimoja cha unga wa molonge katika chakula chao kwa siku. Dk.Samson Tesfay anayseoma Afrika Kusini kwenye chuo kikuu cha Zulu Natal idara inayohusika na masuala ya mbogamboga na matunda,alisema Mlonge ni mmea wenye kutenda maajabu kwenye lishe. "Mlonge ni mmea wa kipekeeunaoweza kuutumia kwa faida nyingi, kama vile dawa, chakula, kuponyesha viungo mwilini na kusaidia kupambana na utapiamlo," anasema. Binafsi nimeshasikia kuwa Mlonge unatibu magonjwa 300, bila ya kusahau kansa,maralia,vidonda vya tumbo,kuondoa sumu mwilini na hata kuongeza nguvu za kiume. Maderava wengi wa safari ndefu hutumia Mlonge kuondoa uchovu. Mlonge watu wa kule Tanga wanatumia kama mti wa kujengea fensi, Uzaramoni umepandwa karibu kabisa na vyoo vyao, Dodoma na Morogoro umejaaa tele. Dar mbegu zake zinauzwa kwa Shilingi 1000 kwa pakti. Mbegu hizo zina dozi ya 3x3x3 na ukizila kwa wingi huweza kukufanya kuhalisha na kutoa uchafu mwilini. Tafakari ndugu yangu dawa za asili tunazo lakini bado tunatumia madawa yenye sumu yaliyotayarishwa na wazungu.... Tafakari.

ARSENAL YAICHARAZA WEST HAM 3-0.

Arsenal ilipata ushindi mzuri dhidi ya West Ham huku ikijiandaa kwa mchuano wa kata na shoka kati yake na kilabu ya Monaco siku ya jumanne. Kilabu hiyo ya Wenger iliishinda West Ham kwa mabao 3-0 na hivyobasi kuimarisha ndoto yake katika nafasi nne bora katika jedwali la ligi ya Uingereza. The Gunner ilitawala mechi hiyo huku Olivier Giroud akifunga bao la kwanza kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika. Kevin Nolan na Matt Jarvis walikaribia kufunga kwa niaba ya wana nyundo hao lakini mabao ya dakika za mwisho ya Aaron Ramsey na Mathiew Flamini yaliiiweka Arsenal pointi nne mbele ya mabingwa wa zamani Manchester United walio katika nafasi ya nne. Arsenal sasa inajianda kubadilisha matokeo ya 3-1 dhidi ya Monaco nchini Ufaransa siku ya jummane katika mechi ya vilabu bingwa barani Ulaya.