Jumapili, 15 Machi 2015

MILIPUKO YALENGA MAKANISA PAKISTAN.

Wasichana walia kufuatia mashambulizi mawili yaliolenga makanisa Pakistan Mabomu mawili yamelipuka yakilenga makanisa mawili yaliyokuwa yamejaa watu kwenye mji wa Lahore chini Pakistan wakati watu walipokuwa wakihudhuria misa ya jumapili. Polisi wanasema kuwa takriban watu 6 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Mashambulizi hayo yanaoyoaminika kuwa ya kujitoa mhanga yalifanyika eneo lenye waumini wengi wa kikristo la YouhanabadH Sehemu ya kundi la Taliban linalofahamika kama Jamatul Ahra limesema kuwa ndilo lililoendesha shambulizi hilo.

BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni