Alhamisi, 12 Machi 2015

MAANDAMANO NCHINI MAREKANI MAAFISA 2 WAPIGWA RISASI.

Maafisa wawili wa polisi wamepigwa risasi huko FURGESON katika jimbo la MISSOURI nchini MAREKANI, wakati wa maandamano katika mji huo. Askari polisi mmoja alipigwa risasi usoni na mwingine begani. Askari wote wanaendelea kutibiwa, na bado haijafahamika ni mtu gani aliyewapiga risasi polisi hao. Idara ya polisi nchini humo imeelezea kusikitishwa na tukio hilo. Kumekuwa na matukio ya mapambano kati ya askari na raia, hasa baada ya watu wenye asili ya AFRIKA kupigwa risasi na kuuawa na polisi, huku wakiwa hawana silaha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni