Jeshi la Nigeria limesema kuwa limegundua kiwanda cha kutengeneza mabomu cha wanamgambo wa Boko Haram katika mji wa Buni Yadi. Wanamgambo waliuteka mji huo ulio kwenye jimbo la Yobe mwezi Agosti lakini jeshi liliudhibiti tena siku ya Jumapili. Msemaji wa wizara ya ulinzi (Chris Olukolade) alisema kuwa mabomu yanayotumiwa na walipuaji wa kujitoa muhanga yalipatikana kwenye kiwanda hicho. Alisema kuwa kiwanda hicho kiko ndani ya jengo linalomilikiwa na kampuni ya mbolea . Boko Haram limetumia mashambulizi ya kujitoa mhanga wakati wa harakati zake za miaka sita za kutaka kubuni taifa la kiislamu kaskazini mashariki mwa nchi.
BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni