Alhamisi, 5 Machi 2015

FAIDA YA BAMIA MWILINI.

Bamia inafahamika kwa wengi katika jamii kwa ladha yake nzuri inapotumika kama mboga katika baadhi ya milo. Wapo wanaoitumia kama kiungo cha mboga na wengine huifanya mboga kamili. Bamia ina majina lukuki, wengine huiita okra, kwa jina lisilo rasmi la Kiingereza huitwa, ‘lady finger’ au gumbo. Bamia ni miongoni mwa mboga za majani ambazo kwa kisayansi huitwa, ‘Abelmoschus Esculentus’ Kwa kawaida hulimwa zaidi kwenye maeneo yenye joto, ukanda wa kitropiki ikiwamo mikoa mikavu kama Dodoma, Singida katika Tanzania. Kwa kawaida huwa na rangi ya kijani iliyokolea na hukua hadi kuwa na urefu wa sentimeta tano hadi 15. Zijue faida za bamia kiafya: Bamia ina wingi wa vitamini A ambayo husaidia kutengeneza kinga ya sumu. Kwa kifupi, sumu inapoingia mwilini bamia huzuia kusambaa kwake. Vitamini A itokanayo na bamia husaidia kuupa mwili wako kinga ya kupigana na maradhi. Kwa wenye matatizo ya kuona, kula bamia mara kwa mara kutaimairisha mwanga katika macho yako. Wingi wa vitamini A huzuia maradhi yatokanayo na virusi kama mafua. Uteute uliomo katika bamia husaidia kuunda tishu za mwili na ngozi. Watu wenye ngozi laini na zinazoteleza wana kiwango kikubwa cha ute ambacho husaidia kujenga ngozi. Ulaji wa mboga za majani kama bamia, husaidia katika kulinda mapafu na saratani za mdomo. Bamia zina wingi wa vitamini K ambayo husaidia kuimarisha mifupa na kuganda kwa damu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni