Aliyekuwa mwenyekiti wa chama tawala Nchini Burundi Hussein Rajabu ameripotiwa kutoroka jela. Hussein Rajabu ambaye alikuwa mwanasiasa mashuhuri nchini humo alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela, mwaka 2007. Rajabu alikuwa anakabiliwa na kosa la hatia ya uhaini dhidi ya serikali kwa kutaka kuzusha vurugu nchini humo. Raia wengi wameonyesha wasiwasi wao kuhusiana na tukio hili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni