Alhamisi, 12 Machi 2015

MTANZANIA ATUNUKIWA TUZO YA UJASIRIAMALI.

Mshindi wa Tuzo za jumla za Pan Commonwealth Julius Shirima akifurahi na washindi wenzake Julius Shirima ni mshindi kutoka Tanzania wa tuzo ya Pan-Commonwealth Youth Award , heshima aliyotunukiwa kwa jukumu lake la kuwawezesha vijana, elimu na usawa wa kijinsia. Bwana Shirima Jumanne jioni pia alitunukiwa heshima ya kuwa mshindi wa tuzo ya Africa Region Commonwealth Youth Award kwa jukumu lake la kumkomboa kijana kiuchumi katika sherehe iliyofanyika jijini London. Aliibuka mshindi kati ya watu 15 walioingia fainali ya kinyang'anyiro hicho. Tuzo hizo zinatolewa kwa vijana wenye umri wa miaka 29 kushuka chini kutoka nchi za Commonwealth kutoka nchi za bara la Afrika, Asia, Pacific, na Caribbean na nchi za Amerika Kusini ambao kazi zao zimekuwa na manufaa kwa watu na jumuia katika nchi zao au ukanda wao. Bwana Shirima, mwenye umri wa miaka 25, ametunukiwa tuzo kwa kuanzisha Darecha, mfuko wa mtaji wa miradi midogo na mtandao wa mjasiriamali ambao unawasaidia vijana wafanyabiashara kubadili dhana ya ujasiriamali kuwa kampuni zenye faida na atapata pauni za Uingereza £5,000 sawa na shilingi milioni 14 za Kitanzania.

BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni