Jumanne, 10 Machi 2015

MLIBERIA;NAKAAJE BENCHI? HAIWEZRKANI.

MSHAMBULAJI wa Yanga, Kpah Sherman, amevunja ukimya akisema hakubaliani na suala la kukaa benchi, lakini anataka kufanya kikao kifupi na kocha wake Hans Pluijm kuhoji kwanini hali iko hivyo. Akizungumza na Mwanaspoti Sherman alisema hafurahii kupewa dakika chache za kucheza ndani ya kikosi hicho ambapo anataka kukutana na Pluijm kutaka kujua tatizo lake nini. “Sijajua nini tatizo katika hii timu naangalia wenzangu wanavyocheza kila kitu naweza kukifanya kuanzia mazoezini mpaka kwenye mechi, naweza kuisaidia Yanga sijajua nini mtazamo wa kocha juu yangu nitazungumza naye ili aniambie nijue,” alisema Sherman ambaye ni Mliberia pekee anayecheza soka Afrika Mashariki kwa sasa. Wakati Sherman akijipanga kukutana na kocha huyo,Pluijm mwenyewe ametoa ufafanuzi juu ya mabadiliko ya timu yake aliyoyafanya katika mchezo dhidi ya Simba juzi Jumapili akisema yalitokana na ugumu wa mabeki wa Simba. “Watu wanaweza kuongea wanachoona, lakini kila kitu kilikuwa wazi tulihihitaji wachezaji wenye nguvu zaidi kuweza kushindana na mabeki na kiungo mkabaji wa Simba, Ngassa alishindwa ndiyo maana tuliwaingiza Javu (Hussein) na Sherman,”alisema Pluijm. Yanga inajiandaa na mechi ya raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Platinum ya Zimbambwe wikiendi ijayo.

GAZETI MWANASPOTI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni