Ijumaa, 6 Machi 2015

DU! KWELI SIMBA TAIFA KUBWA AISEE.

HALI ni tofauti kidogo visiwani hapa baada ya uwepo wa timu kongwe kutoka Bara, Simba, inayojiandaa na mechi dhidi ya Yanga. Uwepo wa Mnyama umelazimisha kusimamishwa kwa michuano iliyokuwa inaendelea katika Uwanja wa Amaan ili kupisha timu hiyo kufanya mazoezi kwani wamelipia uwanja huo kwa siku zote watakazokuwa hapa. Simba ipo visiwani hapa ikijiandaa na mechi dhidi ya Yanga itakayochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam keshokutwa Jumapili ikiwa ni ya raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara. Katika uwanja huo wa Amaan kuna mechi za hatua ya mtoano kwa michuano ya klabu wanachama wa Wilaya ya Mjini lakini jana Alhamisi mechi ya baina ya Zimamoto na Kijangwani ililazimika kusogezwa mbele kuwapisha Simba wafanye mazoezi yao kwani wamelipia uwanja huo. Kocha Mkuu wa Zimamoto, Abdallah Juma ‘Bares’ aliliambia Mwanaspoti ADVERTISEMENT kuwa mechi yao sasa itachezwa wiki ijayo baada ya Simba kuondoka. Simba wanatarajia kurudi Dar es Salaam kesho Jumamosi kama hakutakuwa na mabadiliko. “Simba ni timu kubwa ndiyo maana mechi ambazo zilitakiwa kuchezwa Amaan zimesogezwa mbele, hatujajua ni lini tutacheza ila nafikiri wiki ijayo tutaendelea tunasubiri kufahamishwa baada ya Simba kuondoka,” alisema Bares. Kocha huyo alisema michuano wanayoshiriki inawasaidia katika maandalizi yao ya Ligi Kuu Zanzibar ambayo itaanza muda wowote kuanzia sasa. Ligi hiyo itaendelea baada ya Mahakama Kuu kuamuru viongozi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) walioshitakiwa kuendelea na shughuli za chama hicho isipokuwa marekebisho ya katiba, uchaguzi mkuu na ukaguzi wa mahesabu. Ligi hiyo ilitarajiwa kuendelea hatua ya mzunguko wa pili Januari lakini mpaka sasa bado haijaanza kwani ilisimama kutokana na mzozo uliosababisha kesi mahakamani. ADVERTISEMENT - DESKTOP VIEWBACK TO TOP Soka Makala Za Burudani Kolamu Spoti Majuu Spoti Kenya

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni