SIMBA itacheza na Mtibwa Sugar kesho Jumamosi huku Yanga wakisubiri kuivaa Platinum ya Zimbabwe SIMBA itacheza na Mtibwa Sugar kesho Jumamosi huku Yanga wakisubiri kuivaa Platinum ya Zimbabwe keshokutwa Jumapili, mechi zote zitachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambao juzi usiku yalifanyika matukio ya ushirikina. Uchunguzi uliofanywa na Mwanaspoti umebaini kwamba zinapokaribia mechi za Simba na Yanga, matukio mbalimbali ya kishirikina huchukua nafasi katika uwanja huo. Kuelekea mechi za wikiendi hii, Mwanaspoti imeshuhudia damu kwenye uwanja huo zinazoashiria kuchinjwa kwa mnyama anayedhaniwa kuwa ni mbuzi. Damu hiyo imeonekana katikati ya uwanja huo na inaaminika mnyama husika alichinjwa usiku wa kuamkia jana Alhamisi. Baada ya kumwaga damu yake sehemu mbalimbali, wachinjaji waliondoka naye na kuacha baadhi ya manyoya. Wafanyakazi wa uwanja huo walionekana asubuhi wakifuta damu hiyo kwa maji na hawakutaka kusema lolote.
GAZETI MWANASPOTI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni