Jumapili, 1 Machi 2015

NETANYAHU AFANYA ZIARA YENYE UTATA MAREKANI.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesafiri kuelekea mjini Washington Marekani, katika ziara ambayo amesema ni ya kihistoria katika juhudi za kuzuia mkataba juu ya mpango wa nyuklia wa Iran. Katika ziara yake hiyo yenye utata ambayo itadumu kwa saa 48, Netanyahu atalihutubia bunge la Marekani, katika juhudi za dakika za mwisho kutafuta uungwaji mkono katika kukwamisha makubaliano kati ya Iran na mataifa yenye nguvu kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi hiyo. Ziara ya Netanyahu imeikasirisha vikali Ikulu ya Marekani, na wabunge kadhaa wamesema wataisusia hotuba yake hiyo. Hata hivyo Netanyahu ambaye pia anatazamiwa kulihutubia kongamano la kundi linalotetea maslahi ya wayahudi nchini Marekani, AIPAC, amekaidi miito iliyomtaka kuachana na ziara hiyo, ambayo wengi wamesema imetia doa uhusiano kati ya Israel na Marekani. DW.DE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni