Jumapili, 1 Machi 2015

INASIKITISHA SANA...!ABIRIA MAHUTUTI DEREVA HOI.

Nusu saa iliyopita lmetukia ajali mbaya iliyohusisha bodaboda aina ya boxer karibu kabisa na kona ya sabasaba magengeni mbagala jijini Dar es salaam.

Ajali hiyo imejeruhi vibaya abiria (mwanamke) na dereva wake ambao walikuwa wanatoka mbagala kwa Mangaya  kupitia Kipati kuelekea maeneo ya Temeke  walipofika karibu na kona ya sabasaba,walianguka na kuburuzika vibaya kuliko wasababishia majeraha makubwa.

Majeruhi wote wamekimbizwa hospitali ya Temeke.Cha kustaajabisha ni pale vibaka walipoamua kuingia kazini na kutaka kupora pikipiki,lakini juhudi za askari magereza mstaafu pamoja na mmiliki wa blog hii walihakikisha pikipiki inabakia kwenye mikono salama ya mwenyekiti wa mtaa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni