Jumanne, 10 Machi 2015

AJIBU ANAJUA NYIE ACHENI KABISA.

KOCHA wa Simba, Goran Kopunovic, ameshindwa kuzuia hisia zake juu ya straika Ibrahim Ajibu na kutamka kwamba straika huyo anajitambua na anatambua majukumu yake uwanjani jambo ambalo linampa moyo kuwa anaweza kufanya makubwa. Ajibu amekuwa gumzo mjini kwa wiki kadhaa sasa baada ya kuifungia timu hiyo mabao muhimu ikiwemo mabao matatu ‘Hat Trick’ dhidi ya Prisons wiki moja iliyopita. Kopunovic ambaye aliiongoza Simba kuifunga Yanga bao 1-0 juzi Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu Bara, alisema kwa sasa anatafuta namna ya kumchezesha Ajibu pamoja na straika mwingine ili kufanya vizuri zaidi. “Naweza kusema Ajibu ni miongoni mwa wachezaji muhimu kwenye kikosi changu kwa sasa, anajua kuuchezea mpira, kupiga chenga na kushambulia kwa kasi, ni mchezaji ambaye akijitunza atafika mbali. “Nilijaribu kumchezesha na Emmanuel Okwi kama mastraika wawili wa mwisho kwenye mechi ya Yanga, alifanya vizuri japo muda mwingine alionekana kuwa nyuma kidogo,” alisema Mserbia Kopunovic. Akiwazungumzia Waganda, Dan na Simon Sserunkuma waliosugua benchi juzi, Kopunovic alisema Waganda hao wameshindwa kuwa katika viwango vya juu kiuchezaji.

GAZETI MWANASPOTI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni