KOCHA wa Simba Goran Kopunovic ametamka kwamba kikosi chake kimejaliwa wachezaji wengi wenye KOCHA wa Simba Goran Kopunovic ametamka kwamba kikosi chake kimejaliwa wachezaji wengi wenye vipaji, lakini ndani yake kuna mchezaji mmoja tu mwenye maajabu akimtaja ni Emmanuel Okwi. Kopunovic raia wa Serbia alisema Okwi amekuwa na maajabu ya hali ya juu katika kikosi hicho hasa katika ushindi wa mechi tatu zilizopita ambazo zimethibitisha ubora wake ndani ya timu hiyo. Alisema mabao hayo mawili aliyoyafunga yanatokana na akili iliyotulia aliyonayo mshambuliaji huyo akiwataka wachezaji wengine kuiga. “Anajua nini afanye uwanjani hasa kunapokuwa na mazingira magumu, huo ndiyo ubora wa Okwi ni mchezaji wa kipekee ingawa kuna wengine bora pia,”alisema Kopunovic. “Angalia haya mabao aliyoyafunga katika mechi hizi (dhidi ya Yanga na Mtibwa), kazi kama hii hufanywa na wachezaji majasiri.” Naye mtoto wa Kopunovic aitwaye Denis aliyezaliwa miaka 12 iliyopita aliungana na baba yake kumwagia sifa Okwi. Denis anayeichezea timu moja ya vijana huko Hungary alisema: “Yule mwenye jezi namba 25 ni hatari sana anajua kuwapunguza mabeki angalia anavyobaki na beki mmoja anavyomfanya, anaweza kucheza Ulaya yule.
GAZETI MWANASPOTI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni