Jumamosi, 7 Machi 2015

ALBINO:WAGANGA32 WAKAMATWA.

Polisi nchini Tanzania wamewakamata waganga 32 wa kienyeji kazkazini magharibi mwa jimbo la Geita katika juhudi za kukabiliana na mauaji ya Albino. Siku ya Alhamisi ,watu wanne walihukumiwa kifo kwa mauaji ya mwanamke albino mwaka wa 2008 katika jimbo hilo. Serikali iliwapiga marufuku waganga wa kienyeji mwezi Januari kama mojawapo ya kampeni ya kusitisha mauaji hayo. Waganga wa kienyeji wanaamini viungo vya mwili wa Albino vina nguvu maalum za kuleta mafanikio na bahati. Tanzania imeshuhudia mauaji ya albino 75 tangu mwaka 2000 kutokana na sababu hizo. Afisa mkuu wa polisi katika jimbo la Geita Joseph Konyo ameiambia BBC kwamba waganga hao wa kienyeji walikamatwa na vifaa tofauti ikiwemo dawa za kienyeji na mafuta kutoka maeneo yasiojulikana.

BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni