Ijumaa, 6 Machi 2015
WADUDU WANA VIRUTUBISHO.
Umoja wa Mataifa (UN) umeshauri kula wadudu
wengi ili kukabiliana na janga la njaa. Kwa mujibu wa
ripoti ya Shirika la Chakula na Kilimo la UN, kula
wadudu wengi kunasaidia kuongeza virutubisho
mwilini na pia kupunguza uharibifu wa mazingira.
Tayari watu zaidi ya bilioni mbili duniani wanakula
wadudu kama sehemu ya mlo wao. Hata hivyo, UN
imekubali kuwa bado kuna watu wengi hasa kutoka
nchi zilizoendelea ambao wanaona kinyaa kula
wadudu.
UN imesema kuwa kwa sasa wadudu kama manyigu
na kombamwiko wanatumika kwa uchache sana
kama sehemu ya mlo. Ripoti hiyo imesema kuwa
wadudu wapo kila sehemu na wanazaliana kwa wingi
sana lakini hawatumiki kama chakula.
Waandishi wa ripoti hiyo wanadai kuwa wadudu wana
virutubisho, hasa protini, mafuta na madini. Wanadai
wadudu ni muhimu sana kama chakula hasa kwa
watoto ambao hawapati lishe ya kutosha.
Ripoti hiyo imeshauri kuwa sekta ya chakula inaweza
kusaidia kwenye kampeni ya kula wadudu kwa
kujumuisha recipes mpya za wadudu katika vyakula
vyao na kuongeza wadudu kama menu kwenye
mahoteli.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni