Jumanne, 3 Machi 2015

KUKOMA KWA MAPIGANO UKRAINE BADO NDOTO.

Makubaliano ya kuacha mapigano mashariki ya Ukraine yaligonga Mwamba Viongozi wa Urusi, Ukraine,Ujerumani na Ufaransa wamefanya mazungumzo zaidi kwa njia ya simu kuhusu jitihada za kuhakikisha mapigani yanakoma Mashariki mwa Ukraine. Wamekubaliana kupeleka waangalizi katika maeneo kumi ambako makubaliano ya kusitisha mapigano yalikiukwa ukiwemo Mji wa Shchastya,Volnovakha na maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Donetsk. Viongozi hao wamesisitiza kuhusu uhitaji wa kuwaruhusu waangalizi kufuatilia na kuhakikisha uondolewaji wa Silaha. Petro Poroshenko, Angela Merkel na Francois Hollande kadhalika wamemtaka Rais wa Urusi Vladmir Putin kumuachia huru Nadya Savchenko, Rubani wa Ndege wa Ukraine aliyeshikiliwa tangu mwaka jana, amekuwa katika mgomo wa kutokula kwa siku 80.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni