Jumamosi, 7 Machi 2015

OXFAM:WANAJESHI WA DRC NI WANYANYASAJI.

Shirika la kutoa misaada la Uingereza Oxfam limesema kuwa dhuluma zinazoendeshwa na wanajeshi mashariki mwa jamhuri ya demokrasi ya Congo ni mbaya sawa na zile zinazoendeshwa na waasi. Wanavijiji wamelalamikia kukamatwa bila sababu, kuporwa na kulazimishha kufanya kazi pamoja na kutozwa ushuru kwa lazima. Wengine wanasema kuwa wamelazimishwa kulipa ili kuweza kupitia kwenye vizuizi haramu na kupigwa ikiwa watakataa. Makubaliano na kundi la M23 ya mwaka 2003 yalinuia kuleta amani katika eneo hilo na makundi ya waasi likiwemo lile la FDLR yanaendelea na harakati zao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni