Jumanne, 10 Machi 2015

ZAWADI YA MPUNGA KWA NDOVU SRI LANKA.

Zawadi ya mpunga kwa ndovu Sri Lanka Mzee mmoja nchini Sri Lanka amewakabidhi ndovu shamba la mpunga . Mkongwe wa miaka 75 nchini Sri Lanka, Herath Mudiyanselage Dharmasena, ametwaa hatimiliki ya shamba lake la mpunga na kuwapa watawa wa hekalu ya kibuddha, kwa sharti ya kuwa mazao yote yatakayovunwa kwa shamba hili yapewe ndovu pekee hadi milele. Mpunga hiyo hukuzwa kwa minajili ya ndovu . Sio kwamba jamaa huyu amewapa ndovu urithi kwa sababu amekosana na familia yake, la. Ni kwa sababu ya mapenzi yake kwa ndovu. Na mapenzi hayo yameendelea, licha ya kuwa mmoja wa watoto wake wanane aliuawa na ndovu mwitu. Sherehe ya kufana ya kuwasilisha hati miliki ilifanyika wiki jana karibu na kijiji cha Gedigaswalana, iliyo karibu na mji wa Sigiriya, Sri Lanka ya kati. Kwenye sherehe hiyo, ndovu wawili wa hekalu hiyo waliandamana na washiriki na kukubaliwa kufurahia mazao. Wakazi walifurika kwa wingi kujinea shamrashamra, na mwandishi mmoja wa kinyumbani aliyeshuhudia akisema baadhi ya wakulima waliofika walijawa na machozi ndovu walipoingia mashambani na kuanza kula mpunga. Tukio hili ni nadra katika eneo ambalo migogoro baina ya binadamu na ndovu ni mengi, licha ya kuwa heshima kwa wanyama hawa ni kawaida kwa sababu ya tamaduni za Kibuddha. Wakulima wengi katika eneo hili huwafukuza ndovu kutoka mashamba yao, huku wakiwaona kama tishio kwa maisha yao. Ndovu hao wanalindwa na watawa wa hekalu ya kibuddha. Aidha ni ajabua pia kwa sababu ya kifo cha mwanake Bw Herath Mudiyanselage, aliyeuawa na ndovu akiwa na umri wa miaka ishirini kuendelea. Nduguye marehemu, aitwaye Upatissa, alishuhudia mauaji hayo. “Tulikuwa tukienda zetu nyumbani baada ya kushughulika shambani, kisha tukasikia sauti. Ghafla ndovu akatokea kutoka msituni kando ya barabara. Ndovu huyo akamnyakua ndugu yangu kwa shina lake na kurudi mwituni. Nilianza kupiga mayowe, lakini skuweza kufanya lolote. Nilikimbilia nyumbani, na kumwambia kila mtu. Sote tulielekea mwituni kumtafuta. Mwishowe tukapata mwili wake ukia umeachwa na ndovu huyo. Kichwa chake kilikuwa kimesagwa.’ Upatissa aeleza alikuwa na ghadhabu kubwa na ndovu, kufuatia kifo cha nduguye. Mzee huyo hakueleza kilichopelekea atoe shamba hilo Alielezea BBC kuwa baba yake aliingia kati, na kumwambia kuwa funzo kuu la Buddha ni kuwa mkarimu, hata kwa maadui yako, na kutokuwa na hamaki na yeyote. ‘Baada ya wosia huo hasira ziliisha.’ Upatissa asema licha ya shambulizi hilo, babake bado aliwapenda sana ndovu. Asema pia kuwa baba yake aliona kuw shamba hilo linafaa kuwa la wanyama wa porini, lakini kwamba walikuwa wakililima. Zamani shamba hilo lililkuwa mwitu. Mkulima huyo aliwaeleza wanawe wanaosalia kuwa huu ungekuwa msimu wake wa msiho kulilima shamba hilo. Alifafanua mipango yake ya shamba, na kwamba wote walikubaliana naye. Haikuwa kisa cha mkulima kukosana na kizazi chake. Mbali na hayo, mkewe mkulima aliaga dunia miezi mitatu iliyopita. Kwa hivyo sherehe iliandaliwa kuwa sanjari na tamaduni ya kutoa sadaka Ki BUddhisti, ambayo hufanyika miezi mitatu baada ya kifo cha mtu. Kwa familia inayotegema ukulima, nusu ekari ya shamba la mpunga ni ya thamani kubwa mno, lakini wanawe wasema walitaka kumridhisha baba yao. Mmoja wapo wa wakwe zake, (mkewe Upatissa) alisema hata yeye alitaka kumfurahisha baba mkwe, ingawa walikuwa na watoto watatu pia. Alisema, ‘sisi ni waBuddha halisi, si matajiri wakubwa wala hatujawahi kuwa na mali nyingi, lakini tungali na uwezo wa kupeana chochote kama sadaka. Mzee huyo anaaminika kupenda sana ndovu wa mwituni Mwandishi wa gazeti wa eneo hilo Kanchana Kumara Ariyadasa amesema watawa wa Kibuddha waliotwaa shamaba hilo wanasisitiza umuhimu wa kupokea sadaka kutoka kwa mkulima masikini. BBC ilipojaribu kumpata baba kwa njia ya simu kueleza hadithi yake, mzee alisita kutia fora. Alikuwa ameanza tu sala zake za jioni. Aidha alimwambia mwanaye, ‘mwambie huyo jamaa nitaeleza kila kitu baadaye. Huu ni wakati wangu wa Buddha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni