Jumatatu, 2 Machi 2015

Tanzania inatumia tani bilioni mbili za mkaa kila mwaka ambazo ni zaidi ya Shilingi Trilioni Moja na bilioni 600

Tanzania imekuwa ikitumia zaidi ya tani milioni mbili za mkaa zenye thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni moja na bilioni mia sita kila mwaka fedha ambazo ni nyingi kiuchumi lakini fedha hizo hazijaingizwa kwenye mfumo rasmi unaotambulika na taifa kiuchumi.
Akiongea jijini Dar es salaam mwishoni mwa kongamano la wataalam wa nishati na uhifadhi wa mazingira, mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya kuendeleza nishati endelevu TATEDO,Estomih Sawe amesema fedha zinazotokana na shughuli ya mkaa ni nyingi ikilinganishwa na pato la mazao makuu ya biashara kama pamba,kahawa na chai lakini fedha hizo haizjalinufaisha taifa kiuchumi huku wananchi wa kawaida wanaojishughulisha na uchomaji wa mkaa wakiendelea kuwa masikini na takwimu za shughuli ya mkaa bado ni ngumu kupatikana.

Kwa upande wake afisa mawasiliano kutoka shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania TFCG iliyoandaa kongamano hilo kwa ushirikiano na ubalozi wa USWIS,Betty Luhwuge na mratibu wa mradi wa mkaa endelevu unaotekelezwa katika vijiji nane vya wilaya ya kilosa chini ya TFCG,Chars Leonard wamesema mkaa endelevu unayo manufaa kwa uhifadhi wa misitu lakini pia una tija kwa wananchi wa vijijini na wamesisitiza umuhimu wa kuwepo mipango madhubuti itakayoifanya nishati ya mkaa na kuni iwe na manufaa kwa watanzania kwa miaka mingi zaidi ijayo.

Nae mtaalam wa uchumi, kitengo cha maendeleo ya jamii kutoka ubalozi wa USIWS nchini Tanzania ueli mauderli akiongea wakati wa ufungaji wa kongamano hilo ametoa wito kwa wadau na serikali kushirikiana kikamilifu katika mchakato wa urasimishaji wa biashara ya mkaa na kuwa na mipango endelevu ya uhifadhi wa misitu ta tanzania ambayo ndiyo inayotegemewa kwa uzalishaji wa kuni na mkaa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni