Bwenyenye mmiliki wa kampuni ya kutengeneza kompyuta ya Microsoft , Bill Gates, ndiye tajiri nambari moja duniani kwa mwaka wa pili mfululizo. Kwa mujibu wa takwimu za jarida la Forbes ambalo huchapichwa mara moja kila mwaka bwana Gates ameorodheshwa kumiliki zaidi ya dola bilioni 79.2. Mfanyibiashara kutoka Mexico Carlos Slim Helu ameorodheshwa tajiri nambari mbili duniani na zaidi ya dola bilioni 77.1. Kulingana na jarida hilo,bwana Gates alipata faida kubwa ya dola bilioni $3bn mwaka uliopita Hadi kufikia sasa kuna matajiri 1,826 wenye utajiri unaozidi dola bilioni moja kote duniani hii ikiwa ni ongezeko la mabilionea 181 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Gates ameorodheshwa nambari moja duniani katika miaka 16 kati ya 21 zilizopita. Bwenyenye mwenza kutoka Marekani Warren Buffet anaorodheshwa katika nafasi ya tatu akiwa na dola bilioni $72.7 , Mwanzilishi wa mitindo ya ya nguo ya Zara Amancio Ortega, kutoka Uhispania anashika nafasi ya 4 duniani. Orodha ya matajiri duniani Mwanateknolojia wa Oracle Larry Ellison anashikilia nafasi ya 5. Orodha ya Forbes ya 2015 ya matajiri zaidi duniani. 1. Bill Gates $79.2bn (Microsoft) 2. Carlos Slim Helu $77.1bn (Mfanyibiashara Mexico) 3. Warren Buffett $72.7bn (Mfanyibiashara) 4. Amancio Ortega $64.5bn (Mwanzilishi wa maduka ya nguo ya Zara ) 5. Larry Ellison $54.3bn (Kampuni ya teknolojia Oracle) 6. Charles Koch $42.9bn (Mfanyibiashara) 7. David Koch $42.9bn (Mfanyibiashara) 8. Christy Walton $41.7bn (mmiliki wa maduka ya Walmart) 9. Jim Walton $40.6bn (mmiliki wa maduka ya Walmart) 10. Liliane Bettencourt $40.1bn (Muuzaji wa vipodozi L'Oreal ) BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni