Sudan Kusini imeushtumu Umoja wa Mataifa kwa kutishia kuwawekea vikwazo. Siku ya Jumanne umoja wa mataifa ulipiga kura kuidhinisha azimio linalosema kuwa vikwazo vikiwemo vya usafiri na kupigwa tanji vitawekwa iwapo siku ya mwisho ya kuafikia makubaliano ya alhamisi itapita bila mwafaka. Waziri wa mashauri ya kigeni wa Sudan Kusini Barnaba Marial Benjamin anasema kuwa vikwazo hivyo vitatatiza juhudi za amani na kuathiri watu maskini zaidi nchini humo. Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban ki Moon Amesema kuwa vikwazo hivyo vitachochea mapigano kwa sababu vitazuia maendeleo ya nchi hiyo. Wanajeshi wa serikali watiifu kwa rais Salva Kiir wamekuwa wakipigana vita na wanajeshi wanaomuunga mkono aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar tangu Disemba mwaka 2013.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni