Jumanne, 3 Machi 2015

MAUAJI YA ALBINO NI AIBU KWA TANZANIA.

Raisi wa Tanzania Jakaya Kikwete ameahidi kumaliza kabisa wimbi la mauaji ya Albino,na kusema kuwa waganga wa jadi wanahusishwa na mauaji hayo na kulitia aibu kubwa taifa lake lililoko Africa Mashariki. Wanaharakati wa haki za binaadamu wameeleza kuwa wimbi hilo limechukua uhai wa Albino sabini na tano nchini Tanzania tangu mwaka wa elfu mbili na viungo vyao kutumika katika masuala ya kishirikina. Raisi Jakaya Kikwete amesema kwamba hawezi kuruhusu hali hiyo iendelee kama ambavyo imekuwa ikitendeka kwa miaka iliyopita,haya ameyasema katika mazungumzo yake mapema wiki hii. Rais huyo anaamini katika ushirikiano kati ya serikali na wananchi, vita hii ya kuzuia mauaji ya watu wenye ualbino itafanikiwa kuepuka aibu hii kwa taifa la Tanzania. Inakadiriwa kuwa katika Tanzania nzima kuna Albino wapatao 200,000,na wengi wao hutambuliwa kutokana na rangi yao ya ngozi,macho na nywele zao . Waganga wa kienyeji huwaambia wateja wao kwamba viungo vya Albino huleta bahati ya kupendwa,maisha marefu na mafanikio katika biashara.Imani kama hizo bado zinaendelezwa katika baadhi ya jamii za Ki Afrika ,lakini wanaharakati wanasema kwamba mashambulizi na mauaji ya Albino ni ya kawaida nchini Tanzania. Ni makosa kufikiria kwamba mtu akiwa na viungo vya mtu mwenye u- Albino vitaweza kumsaidia kumletea mafanikio katika biashara, ama atavua samaki wengi na hata kupata madini mengi machimboni .haya ndiyo yanayoendelea katika matendo haya ya kishetani amesema raisi Kikwete. Nchini Tanzanian police mwanzoni mwa wiki hii walizuia maandamano yaliyoandaliwa na chama cha Albino (TAS) yaliyopangwa kufanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Dar es Salaam,kufuatia kifo cha mbunge wa Mbinga Magharibi na pia sababu za kiusalama pia,lakini Raisi Kikwete amekubaliana na chama hicho kukutana na viongozi wa Ma Albino kujadiliana nao njia mwafaka za kukabiliana na mauaji yanayowakabili. Rais Kikwete amesema kwamba zaidi ya maalibo 40 wameshauawa tangu mwaka 2007 lakini amesisitiza kwamba serikali yake inachukua hatua ya kumaliza mauaji hayo . Wauaji wa Albino wamelenga zaidi mikoa yenye migodi ya machimbo ya madini mbalimbali na jamii za wavuvi nchini humo hasa ziwa Victoria ambako Imani hizo za kishirikina zina pewa nafasi kubwa .wanaharakati nao wanadai kwamba wauaji wengi hawaripotiwi vituo vya polisi. BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni