Jumatano, 11 Machi 2015

YALIYOSEMWA NA NADIR HARUB CANAVARO KABLA YA MECHI.

“Kutokana na maandalizi yetu tuliyofanya safari hii ni uhakika, tukiwakosakosa Simba basi ni mabao mawili kwa sababu imani yangu yatakuwa zaidi ya hayo. Nasema hivyo kwa sababu timu kwa sababu timu yetu nzuri kama ulivyoiona. Niko muda mrefu naweza kusema kwa kikosi hiki, kiko vizuri sana,” alisema Cannavaro aliyezaliwa miaka 33 iliyopita mjini Unguja. “Tuna washambuliaji wazuri ambao naamini watafanya kweli. Kikubwa ninachoweza kusisitizia ni umakini tu kwa kuzingatia maagizo tutakayopewa na mwalimu. Lakini umakini pia kwenye safu yetu ya ulinzi, kuhakikisha haturuhusu bao la kufungwa kwa namna yoyote ile,” alisema Cannavaro ambaye amekuwa ni miongoni mwa wachezaji wachache waliokaa na Yanga muda mrefu walioko kikosi cha kwanza.

GAZETI MWANASPOTI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni