Jumatano, 4 Machi 2015

WAMSHITAKI MUGABE KWA KUWAFUTA KAZI.

Wamshtaki Mugabe kwa kuwafuta kazi Mugabe ashtakiwa kwa kuwafuta kazi kiholela rafikize Washirika wawili wa zamani wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe wanamshtaki kwa kuwafuta kazi kiholela. Rigare Gumbo ambaye alikuwa msemaji wa chama tawala cha ZANU-PF na Didymus Mutasa ,katibu mkuu wa chama hicho walifutwa kazi mwezi Disemba na Februari. Walishtumiwa kwa kujaribu kumsaidia aliyekuwa makamu wa rais Joice Mujuru kumpindua rais Mugabe. Waandishi wanasema kuwa mashtaka yao dhidi ya kiongozi huyo wa miaka 91 sio ya kawaida.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni