Rais wa Zambia, Edgar Lungu, ameruhusiwa kutoka hospitali ya Afrika Kusini baada ya kufanyiwa upasuaji. Rais huyo aliyechaguliwa karibuni, ana ugonjwa unaomrejea mara kwa mara, na unaoathiri koo yake. Alilazwa hospitali mjini Pretoria Jumaane. Alizirai katika sherehe za siku ya kimataifa ya wanawake mjini Lusaka. Mwezi wa Januari alishinda uchaguzi wa rais, na kuchukua nafasi ya Hayati Rais Michael Sita, aliyefariki Oktoba mwaka jana.
BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni