Jumatatu, 2 Machi 2015

JONAS MKUDE ACHONGEWA SIMBA.

WANACHAMA wa Simba jana Jumapili walishindwa kuzuia jazba zao na kujikuta wakiweka hadharani mambo ya wachezaji wanayofanya wanapokuwa mtaani wakati wa mapumziko huku kiungo Jonas Mkude akitajwa kuwa ni miongoni mwa hao. Mkude alishitakiwa baada ya Rais wa Simba, Evans Aveva kuruhusu maswali na maoni kwa wanachama wake katika mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, jijin Dar es Salaam baada ya kusoma ajenda yake ya kwanza ya mwendeno wa timu. Mwanachama Nassoro Kigwa mwenye kadi namba 01477 wa Tawi la SMT, Manzese, alimshauri Aveva kuwa wanatakiwa kujenga hosteli haraka ili kupunguza starehe kwa wachezaji ambao wanaendekeza mambo hayo. “Mimi nakaa jirani sana na Mkude ni mchezaji anayeendekeza starehe sana hata tukijaribu kumshauri si mchezaji anayeelewa, tunaomba ili kulinda kipaji chake wawekwe sehemu moja ama kuwajengea hosteli kama ilivyopangwa, Mkude maskani yake ni starehe,” alisema Kigwa. Kwa upande wa Aveva alisema: “Tumesikia maswali, maoni na ushauri wenu tutavifanyia kazi.” GAZETI MWANASPOTI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni