Robo ya wasudan Kusini wameathirika na njaa Shirika la chakula ulimwenguni linasema njaa inaongezeka kwa kasi nchini Sudan Kusini baada ya miezi mingi ya mapigano. Zaidi ya watu milioni mbili unusu wanahitaji chakula cha msaada cha dharura, baada ya kufurushwa makwao kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali na vikosi vya waasi. Mazungumzo ya kuleta amani yaliyokuwa yakiendelea katika taifa jirani la Ethiopia, yamesambaratika. Haya yanajiri siku moja tuu baada ya bunge kumuongeza rais Salva Kiir miaka mitatu zaidi afisini na kuhairisha uchaguzi uliotarajiwa mwaka huu. Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza anaelezea zaidi. Hapa ni katika mji wa Ganyiel kwenye jimbo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Unity, maelfu ya watu waliofurushwa makwao wamefika katika kituo cha Shirika la WFP ambapo wanapata mtama, mafuta na chumvi. Kwa wengi hapa msaada huo ndio chakula cha pekee wakatachopata. Shirika la WFP linasema mtu mmoja kati ya wane nchini humo, hawajui watapata wapi chakula Nchi hii iliepuka kiangazi mwaka uliopita, lakini bado hakuna chakula cha kutosha. Asilimia kubwa ya raia wa Sudan Kusini wanahitaji chakula cha dharura WFP inasema watu milioni mbili unusu wanahitaji msaada wa dharura na idadi hiyo huenda ikaongezeka mara mbili kufikia katikati ya mwaka huu, iwapo mapigano yataendelea. Miongoni mwa wanaopanga foleni hapa kutafuta chakula ni Elizaberth Nyalat aliyetoroka mapigano katika mji wa Nyalat, Kusini Magharibi mwa Nchi hiyo. "nilikuwa nasomea mjini Yei, wakati vita vilipoanza. Nilitoroka Yei hadi hapa. Lakini sio kwa gari wala boti, nilikimbia kwa miguu. Ilikuwa ngumu sana kwangu kufik amahali hapa." Lakini amani hiyo imekuwa ngumu kupatikana. Baada ya miezi kumi na mitano ya mapigano yaliyofanya maeneo mengi kaskazini mwa nchi hiyo kuwa numu kuyafikia. Na sasa mashirika ya kutoa misaada yako mbioni kutoa usaidizi kabla ya msimu wa mvua kuanza. Ertharin Cousin ni mkurugenzi Mkuu wa WFP "watu milioni tatu tunaojaribu kuwafikia,sio tu takwimu ni watu wa kweli. Tatizo ni kuwa , vita hivi vinavyoendelea kwa muda mrefu, ndivyo watu hawa wanasahaulika na kutazamiwa tu kama gharama au takwimu tu. Lakini haya ni maisha ya watu. Ni binadamu." Awamu mpya ya mazungumzo ya amani yanatarajiwa kuanza tena mwezi ujao...lakini huenda ikaathirika na hatua ya bunge hapo jana kumuongezea Rais Kiir miaka mitatu zaidi mamlakani. Uchaguzi wa mwezi Juni pia umeahirishwa. Upinzani hata hivyo unasema hatua hiyo ya Kiir ni sawa na kukwamilia mamlaka. Na huenda ikavuruga juhudi nzima ya kuleta amani nchini humo. Hali hii ya swintofahamu huenda sasa ikamaanisha kuwa kambi za wakimbizi wa ndani kwa ndani zitasalia kuwa makao kwa raia wengi wa Sudan Kusini kwa kuda mrefu zaidi.
GAZETI MWANASPOTI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni