Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu wanne akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha Ihanda wilaya ya Kongwa kwa tuhuma za Mauaji ya vikongwe watatu kwa kuwapiga, kuwaua na kisha maiti zao kuchomwa moto kutokana na imani za kishirikina wakidai kuwa Vikongwe hao walikuwa wanazuia mvua kunyesha katika eneo hilo. Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Sacp David Misime amesema mauaji hayoyamefanyika usiku wa kuamkia tarehe 01/03 mwaka huu kwa nyakati tofauti ambapo tukio la kwanza lilifanyika majira ya saa saba usiku ambapo watuhumiwa wakiwa na silaha mbalimbali Walimvamia kikongwe Saidias Chakutwanga miaka 82 mkazi wa kijiji cha Masinyeti ambaye ni mganga wa kienyeji na kupiga na kitu Kizito kichwani na kisha kumtoboa macho. Watu hao wakafanya tukio la pili siku hiyohiyo majira ya saa nane usiku kwa kuwavamia vikongwe Peter Kaluli miaka 85 na mke wake Kaila kaluli miaka 80 wakazi wa kijiji cha Ihanda na kuwaangushia ukuta wa nyumba waliyokuwa wamelala na kisha kuwachoma moto. Kamanda misime amesema taarifa za awali zinaonyesha kabla ya watu hao kutekeleza mauaji wakiongozwa na mwenyekiti huyo ambaye pamoja na wenzake majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiusalama walifanya kikao cha kuwajadili vikongwe hao Wakiwatuhumu kuzuia mvua kunyeshakatika eneo hilo ambapo hadi hivi sasa jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watuhumiwa wangine waliotoroka. Sambamba na mauaji hayo watuhumiwa hao pia wanadaiwa kuhusika nauharibifu wa mali kwa kuchoma nyumba mbili na kuua mifugo iliyokuwa inamilikiwa na vikongwe hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni