Jumatatu, 2 Machi 2015

US YATISHIA VIKWAZO ZAIDI DHIDI YA URUSI.

US yatishia Vikwazo zaidi dhidi ya Urusi Waziri wa mashauri ya kigeni wa marekani John Kerry ameonya Urusi akisema kuwa itawekewa vikwazo zaidi ikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano mashariki mwa Ukrain hayatatekelezwa kilamilifu. Kerry aliyasema hayo mjini Geneva baada ya kufanya mazungumzo na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov. Bwana Kerry alisema kuwa waasi wanaondoa silaha nzito kutoka sehemu fulani tu ambapo pia wamekataa kuwaruhusu waangalizi wa kimataifa kuingia eneo hilo ili kujionea wenyewe jinsi hali ilivyo. Kerry amesema kuwa ikiwa hali hiyo itaendelea kutakuwa na vikwazo zaidi dhidi ya Urusi ambayo tayari uchumi wake uko katika hali mbaya. Hata hivyo kerry amesema ana matumaini kuwa mazungumzo na mwenzake wa Urusi yataleta sulUhu na kumaliza mapigano nchini Ukrain. Uharibifu uliotokea mashariki mwa Ukraine Bwana Lavrov pia alizungumzia umuhimu wa kutekelezwa kwa makubaliano ya Minsk lakini pia amesema kuwa kuna maendelea na huenda mapigano hayo yakasitiswa. Mkutano huo vilevile unasadifiana na kutolewa kwa ripoti maalum ya Umoja wa mataifa inayoshtumu vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu mashariki mwa Ukraine. UN inasema kuwa zaidi ya watu 6000 wameuawa tangu mapigano hayo yaanze huku mamia wakiuawa katika majuma machache yaliyopita. Bwana Kerry anatarajia kuzua mjadala kuhusiana na mauaji ya kiongozi wa upinzani ambaye pia ni mpinzani sugu wa rais Putin Boris Nemtsov. Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi Sergey Lavrov akiwasili Geneva Kiongozi huyo alipigwa risasi na kuuawa karibu na makao makuu ya urais wa urusi Kremlin siku ya ijumaa iliyopita. Huku hayo yakijiri, Tume ya jumuia ya Bara Ulaya inatazamia kufanya mazungumzo kati ya Moscow na Kiev, ili kutazua tatizo lililoko kuhusiana na usambazaji wa gesi. Juma lililopita kampuni kubwa ya uuzaji gesi, Gazprom, liliwaonya wasambazaji wake kuwa itakomesha pakubwa uuzaji wake wa gesi nchini Ukraine hadi Ukraine kutuma malipo yake ya gesi mwezi huu wa Machi. Aidha mataifa hayo mawili yanatofautiana kuhusiana na usambazaji wa awali wa gesi kwa makundi ya wapiganaji mashariki mwa Ukraine. Mwezi uliopita, Kiev ilisimamisha kutuma gesi hadi katika maeneo yaliyojitenga, ikidai kuwa mabomba ya kupitishia mafuta na gesi yameharibiwa huku kampuni ya Gazprom ikiwasambazia waasi mafuta moja kwa moja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni