Blog hii inapenda kuwatakia heri ya mwaka mpya watanzania wote.
Alhamisi, 31 Desemba 2015
Ijumaa, 12 Juni 2015
ILIVYO PUMU NDANI YA MWILI WA BINADAMU.
Mtu mwenye pumu huwa na mcharuko uvimbe sugu mwilini kwenye mirija yake ya kupitishia hewa (bronchioles tubes) hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija hii na kuwa na ute mzito hivyo kupungua kwa njia ya kupitishia hewa.
Kwa msaada zaidi kama umekumbwa na tatizo hili,ipo dawa ya asili.Piga 0788667736 kwa mawasiliano zaidi.
Ijumaa, 24 Aprili 2015
TOGO KUMCHAGUA RAIS MPYA JUMAMOSI.
Wapiga kura nchini Togo watamiminika vituoni kesho Jumamosi kumchagua rais mpya kwa muhula mingine wa miaka mitano. Rais wa sasa Faure Gnassingbe, ndiye anatarajiwa kuibuka mshindi katika ya wagombea watano. Amekuwa uongozi tangu mwaka 2005 baada ya kumrithi babake ambaye aliitawala Togo kwa miaka 38. Uchaguzi huo unafanyika licha ya kuwepo malalamiko kutoka kwa upinzani na mashirika ya umma kuhusu kutokuwepo mabadiliko ambayo yatapunguza mihula ya rais. Upinzani ulilalamikia uchaguzi wa mwaka 2005 na 2010, ukikishutumu chama kinachoongoza kwa wizi wa kura. Rais wa Ghana na mkuu wa Ecowas Dramani Mahama ambaye aliizuru Togo mara mbili zaidi ya siku 30 zilizopita ametaka kuwepo uchaguzi wa amani. Gnassingbe Eyadema, babake rais wa sasa aliaga dunia mwaka 2005 baada ya miaka 38 uongozini, baada ya kuingia madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1967.
BBC.
WASHUKIWA WA UGAIDI WAKAMATWA ITALIA.
Polisi nchini Italia wanasema kuwa wamewakamata watu 18 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Islamic State kutoka nchini Afghanistan na Pakistan katika oparesheni kubwa ya kupambana na ugaidi. Wanasema kuwa wawili kati ya washukiwa hao wanaaminiwa kuwa walinzi wa aliyekuwa kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden na wengine wanashukiwa kuhusika kwenye mashambulizi nchini Pakistan likiwemo shambulizi lililotokea kwenye soko la Peshawar. Oparesheni hiyo ilikuwa imeendeshwa kwenye kisiwa cha Italia cha Sardina . Polisi walisema kuwa kundi linalofanyiwa uchunguzi lilikuwa limewapangia wanachama wake kuingia nchini Italia wakiwa na vyeti vya kufanya kazi au kama watafuta hifadhi.
BBC.
Alhamisi, 9 Aprili 2015
IRAN YATAKA VITA DHIDI YA HOUTHI KUKOMA.
Rais wa Iran Hassan Rouhani, ametoa wito wa kusitishwa kwa mashambulio dhidi ya wapiganaji wa Kihouthi nchini Yemen, akiyataja kama makosa makubwa. Iran pia imepinga madai ya Saudi Arabia kuwa utawala wa Tehran unawapa wapiganaji hao wa Kihouthi ambao ni wa shia mafunzo ya Kijeshi. Balozi wa Saudi Arabi mjini Tehran, alishutishwa kufika mbele ya wizara ya mambo ya nje ya Iran, kupokea rasmi malalamishi ya Iran. Nchini Yemen, Ndege za kivita za muungano unaongozwa na Saudi Arabia, zimefanya mashambulio zaidi ya anga dhidi ya wapiganaji wa Houthi katika maeneo ya Kaskazini, Kusini na kati kati mwa Yemen. Wapiganaji hao wa Houthi ambao wanapinga utawala wa rais Abd Rabbu Mansour Hadi, wamechukua uthibiti wa maeneo kadhaa nchini humo katika miezi ya hivi karibuni. Akiongea mjini Tehran, rais Rouhani alitaja mashambulio hayo kama makosa makubwa. Awali waziri wa mambo ya nje wa Marekani John kerry alionya Iran dhidi ya kuwaunga mkono wapiganaji hao wa Houthi. Kerry aliyasema hayo baada ya Iran kutuma manuwari mbili za kijeshi katika eneo la Guba la Aden.
BBC.
PALESTINA WAUNGANA NA SYRIA KUWATIMUA IS.
Raia wa Palestina wanasema kuwa wamekubali kushirikiana na serikali ya Syria ili kujaribu kuwafurusha wapiganaji wa IS nje ya kambi moja ya wakimbizi viungani mwa Damascus. Tangazo hilo hilo lilifanywa na afisa mmoja wa serikali ya Palestina huko West Bank. Wapiganaji wa IS walitekeleza shambulizi katika kambi hiyo wiki iliopita na kuweza kuiyumbisha kanbi hiyo licha ya pingamizi kutoka kwa jeshi la Palestina. Takriban wakimbizi elfu kumi na nane wanaishi katika kambi hiyo ambayo inakabiliwa upungufu mkubwa wa vitu muhimu.
BBC.
JAJI NA WAKILI WAPIGWA RISASI ITALY.
Jaji mmoja na wakili ni miongoni mwa watu waliouawa baada ya mshukiwa mmoja kuwafyatulia risasi ndani ya mahakama moja mjini Milan nchini Italia. Maafisa wa idara ya mahakama wanasema kuwa mshukiwa aliyefyatua risasi ni mtu mmoja aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kutangazwa kufilisika. Mshukiwa huyo aliwapiga risasi watu wawili ndani ya mahakama kabla ya kumshambulia jaji ambaye angelisikiliza kesi yake ndani ya ofisi yake. Mtu wa nne anaaminika kufariki kutokana na mshtuko wa moyo. Mshukiwa huyo alikamatwa kaskazini mwa Milan akitoroka kwa pikipiki. Haijulikani jinsi mshukiwa huyo alivyoweza kuingia ndani ya mahakama hiyo huku akiwa na bunduki, kwa kuwa wageni wote hupitia vifaa vya kuwakagua ikiwa wana silaha.
BBC.
MUME 1 KATI YA 10 HUPIGWA NA MKEWE KENYA.
Mmoja kati ya wanaume 10 wa Kenya amepigwa na mkewe ama mpenziwe kulingana na utafiti wa kiafya. Wanaume walio kati ya umri wa miaka 20 hadi 24 ambao ni asilimia 11.7 wamevumilia unyanyasaji huo na wamekuwa wakifuatiwa kwa karibu na wale walio na kati ya umri wa miaka 40 na 49 wakiwa asilimia 9.8. Wale walio kati ya miaka 30 na 39 waliripoti visa vichache huku asilimia 7.1 wakisema kuwa walinyanyaswa kulingana na utafiti huo wa mwaka 2014. Wanaume waliopewa talaka ama hata kutengana na wake zao waliriporti visa vya juu vya unyanyasaji. Walifuatiwa na wanaume ambao wameoa zaidi ya mara moja. Ni asilimia 7.1 ya wanaume ambao wanaishi na wake zao ambao wameripoti visa vya kupigwa. Wale ambao wameoa mara moja walikuwa na visa vichache ikilinganishwa na wale ambao wameolewa mara mbili ama hata zaidi. Wanaume ambao hawakukamilisha elimu ya msingi waliripoti visa vingi vya unyanyasaji wakifuatiwa na wale ambao wamekamilisha masomo ya msingi na yale ya shule za upili..
BBC.
Alhamisi, 2 Aprili 2015
KESSY AGOMEA PESA YA MBOGA.
KATIKA mahojiano baina ya Sekretarieti ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma na viongozi, Profesa Anna Tibaijuka aliyekuwa akituhumiwa kukiuka maadili katika sakata la uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow alitoa kauli moja ambayo iliwafurahisha wengi. Profesa Tibaijuka ambaye ni Mbunge wa Muleba Kusini, alijitetea kwamba matumizi ya Sh10 milioni alizochukua kutoka kwenye akaunti yake baada ya kuingiziwa na mmiliki wa zamani wa Kampuni ya IPTL, James Rugemalira alisema fedha zilikuwa ni kwa ajili ya kununua mboga. Sasa iko hivi; unamkumbuka yule beki wa Simba aliyesajili kutoka Mtibwa Sugar anayekimbiza sana upande wa kulia? Anavaa jezi namba nne. Jamaa naye kagoma Simba anadai hela ya mboga na hayuko kwenye timu hiyo iliyokwenda Shinyanga kucheza na Kagera Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwa alichodai kuwa mpaka wammalizie fedha yake ya usajili iliyobaki na nyumba ya kuishi. Kessy alisajiliwa katika usajili wa dirisha dogo kwa makubaliano ya mkataba wa miaka miwili na dau la Sh 35 milioni na walimpa Sh 20 milioni huku ikibaki Sh 15 milioni alizoahidiwa kulipwa Januari mwaka huu. Simba iliondoka jana Jumatano kuelekea Shinyanga huku Kessy akiwa kwao Morogoro na ameliambia Mwanaspoti kuwa hatarudi Simba hadi viongozi wammalizie fedha ya usajili na nyumba ya kuishi kama mkataba unavyotaka. “Sijaenda na timu, nilirudi kwetu Morogoro tangu Jumapili, unajua haya ni maisha, inauma sana,’’ alisema.
GAZETI MWANASPOTI.
Jumatano, 1 Aprili 2015
UKEKETAJI:DESTURI HARAMU INAYOENDELEA.
Wembe mmoja hutumiwa kwa wote.
Mkeketaji huyu katika kanda ya bonde la ufa nchini Kenya ameshawakeketa wasichana wanne. Wembe alioutumia ni mmoja tu. Tendo hilo la kikatili katika desturi za kipokot linadhihirika wakati ambapo wasichana wanageuka kuwa wanawake. Ukeketaji unakatazwa katika nchi nyingi, ikiwemo Kenya. Hata hivyo, unaendelea - na zaidi katika maeneo ya wafugaji, mbali na miji.
DW.DE
MTU MWENYE UMRI MKUBWA DUNIANI AFARIKI.
Misao Okawa alifariki katika kituo cha uangalizi mjini Osaka,mji ambao alizaliwa mwaka wa 1898. Okawa amewaacha vitukuu sita na wajukuu wanne . Kufuatia kifo chake kuna madai kwamba kumesalia watu wanne pekee wanaodaiwa kuwa hai ambao walizaliwa karne ya kumi na tisa. Wote ni Wanaume huku mwanamume wa mwisho akifariki mwaka 2013.
BBC.
IS YADHIBITI KAMBI YA WAKIMBIZI SYRIA.
IS yadhibiti kambi ya wakimbizi Syria Wapiganaji wa kundi la Islamic State nchini Syria wameingia na kuchukua udhibiti wa kambi kubwa ya wakimbizi wa Palestina ya Yarmouk kandokando ya mji mkuu wa Damascus. Kambi hiyo ambayo ni nyumbani kwa watu elfu kumi na nane imekuwa ikipatikana katika mashambulizi ya udhibiti wa makaazi ya Damscus kati ya majeshi ya serikali na makundi ya waasi ambayo pia yanaipinga IS. Kuna ripoti kutoka ndani ya kambi hiyo kwamba mapigano yanaendelea kati ya wapiganaji wa IS na makundi hasimu. Maafisa wa umoja wa mataifa wameonya mwezi uliopita kwamba wakaazi wa kambi hiyo wanakabiliwa na hali ngumu huku wakikosa umeme,chakula cha kutosha pamoja na dawa.
BBC.
BUHARI AAPA KULITOKOMEZA BOKO HARAM.
WAZAZI WANAPASWA KUDHIBITI UNENE WA WATOTO.
Sheria madhubuti zinapaswa kutungwa ilikuzima matangazo ya kufana ya vyakula vyenye mafuta mengi. Wazazi wengi wanapuuza dalili za mapema kuwa watoto wao wamenenepa kupita kiasi. Madaktari wanasema kuwa wazazi wengi hawajui madhara ya afya kwa watoto walionenepa kupita kiasi. Katika utafiti huo uliowajumuisha zaidi ya familia 2,976 nchini Uingereza ni wazazi 4 pekee waliokuwa na shauku kuwa mtoto wao alikuwa amenenepa kupita kiasi. Madaktari wenye walikuwa wamewatambua watoto 369 kati yao waliokuwa na kiwango cha juu cha mafuta mwilini. Takwimu hizo zinaonesha kuwa watoto walionenepa kupita kiasi sasa wamekuwa kawaida tu majumbani. Watafiti hao wanaonya kuwa hili ni janga kwa afya ya jamii. Asilimia 31% ya wazazi hawajui kutambua dalili za mtoto aliyenenepa kupita kiasi Aidha utafiti huo ulielezea kuwa takriban mtoto mmoja kati ya watano ambao wanaumri wa miaka 6 tayari wanauzito unaozidi kadri kwa asilimia 14%. Kundi hilo la watafiti kutoka taasisi ya usafi ya Uingereza ''London School of Hygiene and Tropical Medicine'' lilizitembela familia 3,000 na kuwahoji iwapo watoto wao walikuwa ni wanene kupita kiasi wastani ama webamba? majibu yao yaliwaduwaza. Takriban thuluthi moja 31% ya wazazi walidunisha uzani wa watoto wao. Proffesa Russell Viner, wa chuo cha Afya ya Watoto aliiambia BBC kuwa wazazi wa kisasa wanamajukumu wengi na hivyo watoto wao hutunzwa na vijakazi asilimia kubwa ya muda ambao wazazi wako makazini mwao. Sheria madhubuti zinapaswa kutungwa ilikuzima matangazo ya kufana ya vyakula vyenye mafuta mengi. ''Hili ni janga ambalo linatokota ,madhara yake yataonekana siku za usoni katika njia ya maradhi mengi tu yanayohusiani na unene'' alisema Professa Viner. Kwa mujibu wa Dakta Dame Sally Davies, ''Afya ya watoto kwa sasa imehujumiwa na dhana kuwa japo mtu ni mnene jamii haitambagua kwani watu wengi duniani ni wanene'' "Nafikiri kwamba itatubidi tuwaelimishe wazazi kuhusiana na maswala ya afya ya watoto wao na pia kuwaeleza kuwa wanapaswa kufuatilia kwa karibu unene au sio wa watoto wao'' Anapendekeza kuwa sheria madhubuti zinapaswa kutungwa ilikuzima matangazo ya kufana ya vyakula vyenye mafuta mengi.
BBC.
Jumatatu, 30 Machi 2015
MATOKEO YA UCHAGUZI NIGERIA LEO JIONI.
Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo ifikapo Jumatatu jioni. Upigaji kura uliendelea katika siku ya pili ya uchgaguzi baada ya kutokea hitilafu katika kadi za kielektroniki na kuchelewesha usajili wa baadhi ya wapiga kura. Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, INEC, Attahiru Jega. "Tumaini letu na ambalo tumekuwa tukilifanyia kazi kwa bidii ni kuweza kutangaza matokeo ya uchaguzi ndani ya saa arobaini na nane na tunatumaini muda mchache zaidi kuliko ule wa mwaka 2011. Imeanza kutoka saa 48 baada ya uchaguzi kumalizika jana. Kwa hiyo tumeanza kuhesabu saa arobaini na nane kwa kweli kutoka jana jioni wakati idadi ya kutosha ya majimbo yalipofanya uchaguzi." Bwana Jega amesema alitumaini jumuia ya kimataifa inaweza kupongeza namna Nigeria ilivyoendesha uchaguzi."Tunaamini tumefanya vizuri kabisa. Hatuwezi kupuuza changamoto tulizokumbana nazo. Ni hakika haukuwa kamilifu lakini tunaamini kwa ujumla tumefanya vizuri sana, japokuwa bado tunayo nafasi ya kuzidi kuuboresha. Na kwa namna yoyote ndiyo maana tuliwaalika waangalizi vikiwemo vyombo vya habari na waangalizi wengine wa uchaguzi, ili kuweza kutangaza habari na tunaweza kujifunza kutokana na ripoti hizi na tunaweza kuendelea kuboresha mchakato wa uchaguzi.", amesema Jega. Wachambuzi wa mambo wanasema ushindani ni mkubwa sana kiasi cha kushindwa kutamka mshindi ni nani. Ujumbe wa waangalizi kutoka Umoja wa Afrika umesema uchaguzi ulikuwa wa amani lakini wamewataka wananchi wa Nigeria kukubali matokeo. Uchaguzi nchini Nigeria umefanyika Jumamosi na Jumapili, ambapo wagombea wawili wa kiti cha urais, Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na Muhammud Buhari kutoka chama cha upinzani cha APC na ambaye katika miaka ya nyuma amewahi kuwa kiongozi wa nchini hiyo wakati wa utawala wa kijeshi wanachuana vikali kuwania kiti hicho.
BBC.
MATOKEO YA UCHAGUZI NIGERIA LEO JIONI.
Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo ifikapo Jumatatu jioni. Upigaji kura uliendelea katika siku ya pili ya uchgaguzi baada ya kutokea hitilafu katika kadi za kielektroniki na kuchelewesha usajili wa baadhi ya wapiga kura. Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, INEC, Attahiru Jega. "Tumaini letu na ambalo tumekuwa tukilifanyia kazi kwa bidii ni kuweza kutangaza matokeo ya uchaguzi ndani ya saa arobaini na nane na tunatumaini muda mchache zaidi kuliko ule wa mwaka 2011. Imeanza kutoka saa 48 baada ya uchaguzi kumalizika jana. Kwa hiyo tumeanza kuhesabu saa arobaini na nane kwa kweli kutoka jana jioni wakati idadi ya kutosha ya majimbo yalipofanya uchaguzi." Bwana Jega amesema alitumaini jumuia ya kimataifa inaweza kupongeza namna Nigeria ilivyoendesha uchaguzi."Tunaamini tumefanya vizuri kabisa. Hatuwezi kupuuza changamoto tulizokumbana nazo. Ni hakika haukuwa kamilifu lakini tunaamini kwa ujumla tumefanya vizuri sana, japokuwa bado tunayo nafasi ya kuzidi kuuboresha. Na kwa namna yoyote ndiyo maana tuliwaalika waangalizi vikiwemo vyombo vya habari na waangalizi wengine wa uchaguzi, ili kuweza kutangaza habari na tunaweza kujifunza kutokana na ripoti hizi na tunaweza kuendelea kuboresha mchakato wa uchaguzi.", amesema Jega. Wachambuzi wa mambo wanasema ushindani ni mkubwa sana kiasi cha kushindwa kutamka mshindi ni nani. Ujumbe wa waangalizi kutoka Umoja wa Afrika umesema uchaguzi ulikuwa wa amani lakini wamewataka wananchi wa Nigeria kukubali matokeo. Uchaguzi nchini Nigeria umefanyika Jumamosi na Jumapili, ambapo wagombea wawili wa kiti cha urais, Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na Muhammud Buhari kutoka chama cha upinzani cha APC na ambaye katika miaka ya nyuma amewahi kuwa kiongozi wa nchini hiyo wakati wa utawala wa kijeshi wanachuana vikali kuwania kiti hicho.
BBC.
FACEBOOK KUFUNGUA HUDUMA MPYA.
Mtandao wa facebook umethibitisha kwamba unafungua huduma yake ya messenger kwa wajenzi .Habari hizo zilitangazwa na Mark Zuckerberg katika kongamano la nane la wajenzi lililofanyika mjini San Fransisco.Zaidi ya programmu 40 mpya zikiwemo habari za hali ya anga tayari zimeandaliwa kwa huduma hiyo.Mtandao huo wa kijamii pia ulionyesha programu yake ya video inayomruhusu mtumiaji kusukuma kamera huku kanda hiyo ikicheza.
BBC.
ARSENAL KUMNUNUA WANYAMA NA MITROVIC.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anapanga kumnunua kiungo wa kati wa Southampton Mkenya Victor Wanyama na mshambuliaji wa Anderlecht Aleksandr Mitrovic kulingana na gazeti la the Sun nchini Uingereza. Wenger amejiandaa kutoa kitita cha pauni millioni 30 kwa wachezaji hao wawili,huku Wanyama akigharimu kitita cha pauni millioni 20 naye mshambuliaji huyo wa Anderlecht Mitrovic akigharimu pauni millioni 10. Inaaminika kuwa Wanyama ataondoka katika kilabu ya Southampton iwapo atachukuliwa na kilabu kikubwa huku naye Mitrovic akiwa amekuwa akifuatiliwa na waajiri wa Arsenal katika kipindi cha wiki chache zilizopotea. Mitrovic amekuwa akifananishwa na Didier Drogba kutokana na mchezo wake.
Jumapili, 29 Machi 2015
RAIA WAANDAMANA KUPINGA UGAIDI TUNISIA.
Raia wa Tunisia wameandamana kupinga ugaidi nchini humo Serikali ya Tunisia inasema kuwa askari wa usalama wamemuuwa kiongozi wa kundi la wapiganaji, lilohusika na shambulio la karibuni dhidi ya makavazi katika mji mkuu, Tunis, ambapo watu zaidi ya 20 waliuwawa. Waziri mkuu Habib Essid alisema, raia wa Algeria, kwa jina Lokman Abu Sakhra ambaye ameelezewa kuwa gaidi hatari kabisa nchini humo aliuwawa, pamoja na wapiganaji wengine wanane, kwenye shambulio lilofanywa katika jimbo la Gafsa, magharibi kwa nchi. Wapiganaji hao ni wa kundi liitwalo Ibn Nafaa Brigade. Maelfu ya watu wameshiriki kwenye mha-dhara wa mshikamano, kupinga ugaidi. Watu maarufu walishiriki kwenye mhadhara huo, pamoja na wageni mashuhuri, akiwemo Rais François Hollande wa Ufaransa, Waziri mkuu wa Itali, Matteo Renzi, na kiongozi wa Wa Palestina, Mahmoud Abbas.
BBC.
UPIGAJI KURA WAENDELEA NIGERIA.
Shughuli ya kupiga kura yaendelea katika maeneo kadhaa nchini Nigeria Katika uchaguzi mkuu wa Nigeria, watu wanaendelea kupiga kura kwa siku ya pili katika baadhi ya vituo, kwa sababu ya matatizo ya kiufundi yaliyotokea jana. Vifaa vya kusoma vitambulisho, vilivyokusudiwa kuzuia udanga-nyifu, viliharibika, na kuchelewesha upigaji kura. Lakini katika maeneo mengine, mamilioni ya wa Nigeria walipiga kura bila ya tatizo. Mashindano ni makali baina ya wagombea wawili wakuu wa urais, Goodluck Jonathan na kiongozi wa zamani wa kijeshi, Muhammadu Buhari. Wanajeshi wa Nigeria hivi sasa wanapambana na wapiganaji kadha wa Boko Haram, nje ya mji wa Bauchi, kaskazini-mashariki mwa nchi.
BBC.
Jumamosi, 28 Machi 2015
SIMBA YAGUNDUA UCHAWI WA MSUVA.
WAKATI Simba wakiweweseka na kasi ya mabao aliyonayo Simon Msuva wa Yanga, kinara huyo wa mabao wa Ligi Kuu ni kama amewafichulia siri yake. Msuva mwenye mabao 11, matano kati ya hayo akiyafunga kwa kichwa, mawili kwa penalti na manne kwa mguu alifichua kuwa wala si uchawi kama watu wanavyofikiria bali ni ujanja wake wa kuiba muda wa kocha wake, Mholanzi Hans Pluijm wanapokuwa mazoezi ili kujifunza kufunga ndiyo sababu ya kumfunika Didier Kavumbagu mwenye mabao 10. Aliweka wazi kuwa, amekuwa akiwasumbua, Juma Abdul na Mnyarwanda Mbuyu Twite mara kwa mara wampigie mipira ya krosi na yeye amalizie kufunga kwa kichwa au mguu huku makipa, Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ally Mustapha ‘Barthez’ akiwaomba wakae golini. Alisema, amekuwa akifanya hivyo karibu kila kipindi cha mazoezi na kila mmoja amekuwa anamwomba ampigie mipira mitano au sita na kwa upande wa makipa mbali na kuokoa mipira hiyo ya krosi, huwa anawapigia mipira mingine mitano ya penalti kila mmoja. Akizungumza na Mwanaspoti, Msuva alisema: “Ninatamani kufunga, napenda nifunge na hamu yangu ni kufunga lakini pale ninapoweza faida ya klabu na mimi mwenyewe, nikawa nafanya sana mazoezi ili nifanikiwe.” “Nimekuwa nikiwasumbua sana baadhi ya wachezaji mazoezini, huwa naibia mwalimu anapokuwa amesimamisha programu yake kwa muda mfupi, huwa nawaomba wanipigie krosi na mimi nijaribu kufunga kwa kichwa na miguu makipa wakiwa golini. Wakati mwingine nawaomba pia wachezaji wa katikati wanichezeshee mipira nayo nafunga ni hivyo tu,” alisema Msuva ambaye amefunga mabao ya kichwa katika mechi waliyocheza na Prisons mzunguko wa kwanza bao moja, raundi ya pili mawili dhidi ya Prisons, moja na Mbeya City na moja dhidi ya Azam. “Lakini pamoja na hamu yangu hiyo, huwa silazimishi kufanya hivyo, ninapokuwa sina uwezo, pia namwomba Mungu anilinde na majeraha ili nitimize malengo yangu ya kufunga kadri niwezavyo ili niwe mfungaji bora na timu yangu ichukue ubingwa.” Msuva ambaye kuna habari kwamba Simba inamuwania pia aling’ara kwa mabao kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi ambalo hata hivyo ni mahasimu wao Simba ndio waliobeba taji la michuano hiyo.
REKODI
Awali Msuva alikuwa anacheza straika wa kati katika klabu mbalimbali alizopitia kama, Azam FC, Moro United na timu za Taifa za vijana chini ya miaka 17 na 20. Baada ya kutua Yanga, alihamishiwa pembeni nafasi ya winga na yeye anasema: “Sina tatizo kucheza nafasi hiyo, kama una uwezo wa kufunga mabao, kokote utafunga iwe straika wa kati au winga pembeni.” Kocha wake mkuu, Mholanzi Hans Pluijm amesifu kiwango cha Msuva kuwa ni mchezaji anayefuata maelekezo na kukubalia mabadiliko. Umahiri wa Msuva unakaribiana na ule waliokuwa nao wachezaji Mrisho Ngassa na Mussa Hassan Mgosi ambao ni mawinga, lakini walioweza kunyakua tuzo ya Ufungaji Bora katika Ligi ya misimu ya nyuma kwa kufunga mabao 16 kila mmoja katika msimu wake. Kasi hiyo ya Msuva kwa mechi saba zilizosalia kwa timu yake kabla ya kufunga msimu inaweza kumfanya amfikie aliyekuwa Mfungaji Bora msimu uliopita Amissi Tambwe aliyefunga mabao 19. Hata hivyo, uwiano wake wa mabao unampa wakati mgumu kufikia rekodi hiyo ya Tambwe aliyemzidi mabao mawili Kipre Tchetche aliyekuwa kinara wa mabao msimu wa 2012-2013.
GUMZO MWANZA
Wakati nyota wa Yanga wakitua jijini hapa kwa ajili kambi ya Taifa Stars inayojiandaa kucheza na Malawi kesho Jumapili, Msuva amekuwa gumzo midomoni mwa mashabiki wa soka wa Mwanza baada ya kutoonekana kwenye mazoezi na wenzake. Mashabiki wameingiwa na mchecheto na kuhoji alipo Msuva na kudai kama hatakuwemo ni wazi Malawi itakuwa na kazi rahisi kushinda. Wachezaji wa Yanga walionekana kambi ya Stars ni Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Mrisho Ngassa waliotua juzi Alhamisi, walipasha kidogo uwanjani kabla ya kuondoka na gari la Meneja wa Uwanja wa CCM Kirumba na Kocha wa Toto Africans, John Tegete. “Tumefurahi kuwaona nyota wa Yanga wakijumuika na Stars, lakini hatujaridhika na tuna mashaka makubwa kwani hatujamuona Msuva na muda wa mazoezi ni mdogo sijui kama wataweza kuwahimili wa Malawi,” alisema Selemani Mashimba. Hakuna kiongozi wala kocha aliyekuwa tayari kuzungumza jambo lolote la timu hiyo kwa madai watazungumza siku moja kabla ya mchezo. Katika mazoezi ya juzi ya mashabiki iliongezeka na kama Chama cha Soka Mwanza (MZFA) wangeamua kuwatoza kiingilio cha Sh1000 basi wangepata pesa za maana. Mashabiki wengi walikuja ili kuwaona nyota hao wa Yanga tofauti na hali ilivyokuwa katika mazoezi yaliyopita. Hata hivyo, wakati mashabiki wakiwa na hamu na Msuva, strika Mbwana Samatta aligeuka kivutio kikubwa kwenye upigaji wa penalti katika mazoezi hayo ya juzi baada ya kumtungua Mwadini Ally kwa mikwaju saba jambo lililomfanya kipa huyo abaki akicheka tu.
GAZETI MWANASPOTI.
Ijumaa, 27 Machi 2015
YANGA YAMJAZA UPEPO STRAIKA WA SIMBA.
VIONGOZI wa Simba, wamegundua kwamba walibugi kumpiga chini straika wao namba moja wa msimu uliopita, Amissi Tambwe ambaye sasa anatamba na kuwapa kiburi Yanga kutokana na uwezo wake wa kutupia kwenye nyavu. Vigogo hao wameingia msituni kumsaka mchezaji huyo kwa udi na uvumba ili arudi Msimbazi haswa baada ya Kocha Mserbia, Goran Kopunovic kuwaambia mabosi wake kwamba mchezaji huyo bado ni kifaa na anamhitaji. Lakini Yanga wamemuweka chini Tambwe na kumwambia atulie watampa maisha bora na kitendo cha timu hiyo kushiriki michuano ya kimataifa ndicho kimempagawisha zaidi aendelee kubaki Jangwani ambapo amemhakikishia Kocha Hans Pluijm kwamba harudi Simba hata kwa dawa. Akizungumza na Mwanaspoti, Pluijm ambaye ni Mholanzi, amesema amezungumza na Tambwe juu ya maisha yake ya baadaye ambapo raia huyo wa Burundi amemhakikishia kwamba hawezi kurudi Simba msimu ujao. Pluijm alisema Tambwe ambaye mpaka sasa ameshaifungia Yanga mabao saba katika mashindano ya aina mbili bado ni mchezaji muhimu katika kikosi chake baada ya kukubalika katika mfumo wa timu hiyo. “Nimesikia hizo taarifa kwamba kuna watu wanataka kumrudisha Simba, nikazungumza na Tambwe na amenihakikishia kwamba hawezi kukubali kurudi huko tena kwani anafuraha akiwa hapa na timu yetu, jambo zuri ni kwamba Tambwe ni mchezaji wetu anayefanya vizuri nafurahia anavyojituma katika timu ameweza kufanya kile ambacho makocha tunamtaka afanye uwanjani, katika hilo unawezaje kumruhusu mtu kama huyo aondoke katika timu yako?” alisisitiza Pluijm. Hata ushiriki wa Yanga kwenye michuano ya kimataifa umemfanya mchezaji huyo kutuliza akili Yanga kwa madai kwamba mbali na kushiriki msimu huu kwenye Kombe la Shirikisho hata mwakani kuna uwezekano mkubwa wa kushiriki tena huku nafasi ya Simba ikiwa finyu kutokana na kuchechemea kwenye ligi ya ndani. “Sijajua kwa nini Tambwe aliachwa, anafanya vizuri tunahitaji mtu kama huyo katika timu yetu, ukiangalia kwa sasa tuna mtu mmoja tunayemtegemea katika ufungaji Okwi, anakosa msaidizi, namjua vyema Danny (Sserunkuma ) lakini ameshindwa kufanya vizuri,”alisema Kopunovic. “Nilikuwa mshambuliaji, namjua mshambuliaji mzuri, angalia Chelsea walikuwa na shida ya ufungaji wakamsajili Diego Costa sasa anafunga, siku zote mchezaji mzuri ni yule anayefanya vizuri katika wakati husika,”alisisitiza kocha huyo ambaye kuna uwezekano mkubwa akamtema Sserunkuma ambaye tayari ameshaomba kupunguza urefu wa mkataba wake aondoke Simba baada ya mambo kutomwendea vizuri.
GAZETI MWANASPOTI.
Alhamisi, 26 Machi 2015
A GIRL WITH POSITIVE IDEA.
My boyfriend and I both have a lot on our plates. He with his work, which is crazy intense, and me with my work and studying for licensure. Despite all this pressure and chaos, we still make time for each other on the weekends and a few hours throughout the week. We both commented on that fact tonight how despite everything we are still going strong. I guess we're important to one another and both willing to find a way rather than finding an excuse to run away.
NINI KILIIKUMBA NDEGE YA UJERUMANI?
Wakaguzi wa kifaransa wamesema wamefanikiwa kukipata kifaa cha kurekodia sauti na maneno kutoka katika kisanduku cheusi cha ndege ya shirika la ndege la ujerumani iliyopata ajali katika milima ya Alps. Wakaguzi hao mpaka sasa wanaendelea kukitafuta kisanduku kingine ,ambacho hurekodi taarifa za ndege hiyo na chanzo cha ajali hiyo . Timu hiyo ya uokozi iliyoko katika eneo la ajali lililoko upande wa Kusini mwa Ufaransa wamefanikiwa kukipata kifaa hicho kinachohifadhiwa katika chumba cha rubani kikiwa kimeharibika. David Gleave ni mkaguzi wa zamani wa ajali za ndege ,anasema kwamba visanduku hivyo vinapaswa kuwa na picha dhahiri za nini kilichotokea . pengine tunaweza kupata mawasiliano ya timu ya wafanya kazi wa ndege hiyo,ambayo yatatuelekeza katika kilichojiri na chanzo cha tatizo ambalo walijaribu kulitatua pamoja kama timu,na hatua walizochukua kunusuru janga hilo. Je rubani alichukua juhudi za makusudi kuwanusuru abiria na wafanyakazi waliokuwemo,na rubani mwingine aliendelea kurusha ndege? Ama kutatua tatizo?na namna walivyohakiki na nini walichokiacha na mambo kama hayo. nini kilitokea? swali halina jibu,kisanduku cheusi kimeharibika Hata hivyo tunahitaji zaidi taarifa za kinasa taarifa ili tuweze kupata mustakabali kamili wa kile kilichotokea. Akizungumza katika mkutano na waandishi habari Carsten Spohr ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege la Germanwings shirika dada la kampuni ya usafirishaji ya Lufthansa ameielezea ajali hiyo kuwa isiyoeleweka. niamini baada ya miaka ishirini ijayo katika tasnia hii nami niliwahi kuwa rubani wa shirika la ndege la Lufthansa,bado hainiingii akilini juu ya kile kilichotokea jana. Shirika la ndege la Lufthansa halijawahi kupoteza ndege yake katika historia yake ya usafirishaji katika mazingira kama hayo ,bado hatuelewi nini kiliisibu ndege iliyokuwa katika hali nzuri kiufundi na marubani wawili waliobobea katika kazi yao na waliopitia mafunzo ya hali ya juu ya safari za anga wa shirika la Lufthansa,kuhusika katika ajali mbaya kiasi kile .
BBC.
MAREKANI:Uganda hatarini kushambuliwa.
Ubalozi wa Marekani nchini Uganda, umesema una taarifa za uwezekano wa shambulio la kigaidi nchini humo. Aidha Marekani pia imetoa tahadhari kwa raia wake. Taarifa ya ubalozi huo umebainisha kwamba shambulio hilo linaweza kutekelezwa wakati wowote, katika maeneo ambayo raia wa mataifa ya Magharibi na Marekani hukutana. Katika kipindi kilichopita, kundi la Al-Shaabab lenye makao yake Nchini Somalia, limetekeleza mashambulio Nchini Uganda.
BBC.
Jumatano, 25 Machi 2015
NIGERIA YAKIRI KUTEKWA NYARA RAIA.
Serikali ya Nigeria imekiri kwamba raia,wakiwemo watoto wametekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram katika majuma ya hivi karibuni. Msemaji Mike Omeri amesema kuwa ni vigumu kukisia idadi ya watu ambao wametekwa wakati wapiganaji wa Boko Haram wakitoroka wakati wa mashambulizi dhidi yao yanayotekelezwa na vikosi vya kijeshi kutoka Nigeria,Chad na Niger. Lakini msemaji wa Nigeria alipinga madai kwamba zaidi ya watoto 500 walikuwa hawajulikani waliko kutoka mji uliochukuliwa na jeshi Damasuk karibu na mpaka wa Niger. Nigeria imetangaza kwamba inafunga mpaka wake kuanzia siku ya jumatano usiku hadi jumapili huku uchaguzi wa urais ukifanywa.
BBC.
MABIBI HARUSI WA ZAMANI ZIMBABWE WAONGEA.
Mabibi harusi wa zamani wawili wameamua kuipeleka serikali ya Zimbabwe mahakamani katika harakati za kuvunja sheria kandamizi nchini humo na kutaka sheria inayoruhusu mabinti kuolewa wakingali wadogo iwe ni kinyume na katiba na si halali kwa kifupi iharamishwe. Mabibi harusi hao Loveness Mudzuru na Ruvimbo Tsopodzi wamesema ndoa za utotoni ,ambazo ni ruksa nchini Zimbabwe,wansema ni sawa na ukatili wa kijinsia kwa watoto ambao huwanasa mabinti na kuishia katika janga la umasikini na madhila yasiyosemeka. Nimekabiliana na changamoto zisizosemeka ,mume wangu alikuwa akinipiga sana.nilikuwa natamani kuendelea na masomo lakini yeye alikataa.nilikuwa na hali mbaya sana huu ni ushuhuda wa Tsopodzi, mama wa mtoto mmoja,mama huyu aliolewa akiwa na umri wa miaka kumi na mitano tu . Na anaendelea kusema kwamba anataka kuchukua hatua hiyo ili kuleta tofauti,ameeleza hayo akiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare mapema wiki hii.Na hii yote ni katika harakati za kuzuia mabinti wadogo wanaoolewa katika umri mdogo. Takwimu zilizochapishwa mwaka wa jana zinaonesha kwamba moja ya tatu ya wasicha walio na umri wa chini ya miaka kumi na nane huolewa , wakati wengine wapatao asilimia tano huolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka kumi na mitano. Katika tamko lao kwa mahakama ya katiba, Tsopodzi na Mudzuru, ambao kwa sasa wana miaka 19 na mwingine ana miaka 20, wanasema kwamba sheria ya ndoa nchini Zimbabwe ni ya kibaguzi kwani inamtaka mtoto wa kike aolewe akiwa na umri wa miaka kumi na sita wakati mtoto wa kiume anatakiwa kuoa akishatimiza umri wa miaka kumi na nane, na ndoa za kimila hazijaainisha umri halisi wa kijana ama binti kuoa ama kuolewa. Sheria ya ndoa ya mwaka 2013 inasema kwamba kila mtoto mwenye umri wa miaka kumi na mitatu,anayo haki ya kupata malezi ya wazazi,elimu na ulinzi kutoka kwao katika masula ya unyonyaji kingono na kiuchumi. Sheria hii pia haijaweka wazi umri wa kuoa ama kuolewa lakini inasisitiza kwamba hakuna mtu yeyote atakayelazimishwa kuoa ama kuolewa kinyume na matakwa yao na kuonesha wazi kuwa raia wa Zimbabwe mwenye umri wa miaka kumi na nane anaweza kuwa na familia yake. Umasikini ndio chanzo cha ndoa za utotoni nchini Zimbabwe na kuwasababisha kuolewa kabla ya umri wao wasichana walio wengi ,na hivyo kuwasababisha wazazi kupunguza mzigo wa familia katika masuala ya matunzo na kubakisha mama tu na baba.ulipwaji mahari nayo ni motisha inayowafanya wazazi kutowatendea haki watoto wao. Baadhi ya familia nchini Zimbabwe zinatukuza ndoa za utotoni kwa mtazamo wa kuwalinda watoto wao wa kike na ngono kabla ya ndoa. Mudzuru anatoa ushuhuda wake kwamba ndoa za utotoni ni chagamoto kubwa ,kwani mabinti hao walio katika umri mdogo watazaa watoto wakiwa katika familia masikini na hapo ndipo mzunguuko wa ndoa za utotoni unapoanza upya. Mudzuru, aliolewa akiwa na umri wa miaka kumi na sita kwa sasa ana watoto wawili tena akiwa hajatimiza miaka kumi na nane ,anasema maisha yake yalikuwa sawa na jehanamu ya moto na aliishi maisha yake katika dhiki isiyosemeka. Nasema maisha yake yalikuwa magumu sana, kulea watoto ilhali wewe mwenyewe ukiwa ni mtoto ni vigumu,na asema katika umri wake alipaswa kuwa anahudhuria masomo shuleni. Naye mwanasheria wa mabinti hao ambao ni akina mama sasa hivi,alikuwa ni waziri wa zamani wa fedha nchini humo Tendai Biti, aliwasilisha changamoto hizo za kisheria mwezi January mwaka huu. Beatrice Savadye,yeye ni mwanaharakati wa kupinga ndoa za utotoni nchini humo anayeongoza asasi isiyokuwa ya kiserikali,ijulikanayo kaka ROOTS ,asasi ambayo inawaunga mkono akina mama hao wawili anasema kesi hiyo imekuwa na mvuto wa kipekee nchini humo nan je ya nchi hiyo kwa ujumla wake. Na anamashaka kama mahakama itatoa maamuzi yake lini ,lakini inalazimika kutoa maamuzi yake ndani ya miezi sita. Ulimwenguni kwa ujumla wake wasichana milioni kumi na tano wanaolewa kila mwaka.katika jangwa la sahara peke yake asilimia arobaini ya wanawake huolewa wakiwa katika umri mdogo.
BBC.