Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila jijini Dar, Gaudensia Albert. HII ni simulizi ya aibu! Tukio la mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila jijini Dar, Gaudensia Albert, mkazi wa Kisiwani Kata ya Sandali wilayani Temeke kuishi na vinyesi, mikojo na matapishi chumbani kwake, limeibua mshtuko na aibu ndani yake. Kwa mujibu wa mwenye nyumba, Reuben Shayo, mwalimu huyo anayefundisha masomo ya sayansi aligundulika hivi karibuni kuwa anaishi ndani ya chumba chenye rundo la uchafu huo. Shayo alifunguka: “Siku ya tukio (Februari 22, mwaka huu) tuliona funza wakitoka chini ya mlango wa ticha na harufu mbaya. “Ukweli ni kwamba mwenzetu hatujawahi kumuona akioga wala akiingia chooni, ndiyo tukabaini uchafu huo baada ya kuchungulia ndani. “Yaani hakuwahi kuleta mgeni wa aina yeyote na kumwingiza ndani hivyo inaonesha dhahiri alikuwa akiogopa kuonesha uchafu wake.” Umati wa watu waliokusanyika katika eneo la tukio. Baada ya kugundulika kuwepo kwa uchafu huo, Shayo na wakazi hao walitoa taarifa polisi ambapo awali, Sajenti wa Jeshi la Polisi, Ramadhan Kagolo, aliwajibika kusimamia kuvunjwa kufuli la chumba hicho kwa vile kazi iliyokuwa ikifanyika ilikuwa ni kwa ajili ya kulinda afya ya jamii. Jumatano iliyopita, Manispaa ya Temeke ilichukua uamuzi wa kuteketeza kinyesi kilichokutwa katika chumba cha mwalimu huyo baada ya maofisa wa afya wa manispaa hiyo kutaka kunusuru afya za wakazi wa eneo hilo. Wakitoa kinyesi hicho nje. Kazi hiyo ilifanyika majira ya saa 9:00 alasiri chini ya uangalizi wa jeshi la polisi kwa kushirikiana na mwenyekiti wa mtaa huo, Yahya Bwanga. Wakati wa tukio hilo, Ofisa Afya wa Manispaa ya Temeke, Floyd Tembo alisema baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa tukio hilo la kushangaza, waliwatuma watendaji wa afya wa kata hiyo wafanye utafiti wa kujua tatizo lina ukubwa gani. “Baada ya kufanya utafiti wao pia walimpata mhusika ambapo tulichukua jukumu la kwenda kumhoji mkuu wa shule hiyo ili kujua kama mwalimu Gaudensia alikuwa na akili timamu au la. “Hata hivyo, mkuu huyo wa shule alitueleza kuwa ana akili timamu na kwamba tukio hilo limewashtua walimu wenzake,” alisema Tembo. Alisema pamoja na kuuteketeza mrundikano huo wa kinyesi, bado wanaendelea na utaratibu wa kumfikisha mwalimu huyo kwenye vyombo vya sheria ili kujua kwa nini alifanya hivyo. “Hili tukio halihusiani na ugonjwa wa akili inawezekana kuna tatizo lingine au labda mambo ya ushirikina, haiwezekani ajisaidie na kuhifadhi uchafu ndani kwake,” alisema. Alisema mwalimu huyo hakuweza kufika kwenye eneo la tukio hali iliyofanya mlango wa chumba chake uvunjwe chini ya uangalizi wa polisi. Tembo alisema mwalimu huyo alishindwa kutokea kwenye eneo la tukio kwa vile alipelekwa Hospitali ya Temeke kisha kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kupimwa afya baada ya kupata mshtuko ambao umesababishwa na taarifa hizo. Afisa Afya wa Usafi wa Mazingira wa Temeke, Jumanne Muhogo alisema uchafu walioubaini ulikuwa ni uchafu wa kinyesi, mkojo na matapishi inasemekana kuna kipindi alikuwa anatapika. “Tukio hili kwa Manispaa ya Temeke ni la kwanza kutokea, inaelekea huyu mtu hana akili ya kawaida kama angekuwa na akili ya kawaida asingeweza kufanya namna hii,” alisema. FARAJI MFINANGA.
Jumamosi, 28 Februari 2015
AZAM NJE KLABU BINGWA BARANI.
Timu ya Azam FC yenye maskani yake nje kidogo ya jiji la Dar es salaam,leo lmepigwa jumla ya mabao matatu bila majibu na timu ya El merreikh ya sudan katika mchezo wa marudiano ambapo mchezo wa awali azam ilishinda nyumbani 2-0.
Kwa mantiki hiyo,tayari azam imeshafurushwa katika mashindano hayo kwa jumla ya mabao 3-2.
KAPTENI JOHN KOMBA AAGA DUNIA
Mbunge wa Mbinga magharibi,mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm yaifa na kiongozi wa TOT bendi kapteni John komba ameaga dunia leo hii katika haspitali ya TMJ jijini Dar es salaam.
MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI...AMEN!
HUWEZI KUISIFU WALA KUIPONDA SIMBA.
Timu ya simba leo imeibomoa prisons ya mbeya kwa mabao matano bila majibu.
Ibrahim ajib akitupia matatu(hat-trick).Okwi akitupia la nne na la tano liliwekwa kimiani na Ramadhan Singano.
Ushindi huu wa Simba usiwe kiini macho cha mkutano wa kesho ajenda zijadiliwe kama ilivyokusudiwa ili simba isonge mbele na kuwatoa mashabiki wake kimasomaso.
AZAM WAJANJA SANA AISEE.
TUMEPITA.
KIPATO huleta majivuno. Ni usemi maarufu wa Kiswahili unaoweza kutumika kutafsiri kipigo cha mabao 2-1 ilichopata ugenini dhidi ya BDF XI kwenye mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho. Lakini hiyo haiondoi Yanga kuitwa Wanaume wa Shoka kutokana na ugumu wa michuano hiyo. Yanga ilishinda mabao 2-0 kwenye mchezo wa awali jijini Dar es Salaam, matokeo yaliyoipa kiburi kiasi jana Ijumaa ikacheza kwa mbwembwe zilizosababisha matokeo hayo ingawa mwamuzi naye alitoa kadi za njano ambazo ziliwapa mchecheto wachezaji wa Yanga. Hata hivyo imesonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 ikibebwa na ushindi wake wa kwanza. Yanga ilitumia sekunde 1800 ambazo ni dakika 30 kupata bao la kuongoza lililofungwa kwa kichwa kupitia kwa kiraka mwenye kasi Mrisho Ngassa ambaye alipokea pasi ya Amissi Tambwe aliyeituliza kwenye boksi krosi safi ya Msuva. Bao hilo liliwachanganya wenyeji ambao kipindi chote cha kwanza hawakupiga hata shuti moja la maana. Kipindi cha pili ambacho wachezaji wa Yanga walionekana kuzidiwa na hali ya hewa ya baridi, Moreetsi ‘Resco’ Mosimanyana aliipatia bao BDF dakika ya 46 kupitia krosi ya Pelontle ‘Dust’ Lerole ambayo ilimshinda kipa Ally Mustapha ‘Barthez’ aliyeonekana kusumbuliwa na mipira ya juu hususani kipindi cha pili. Dakika ya 69 Danny Mrwanda alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kucheza rafu mbaya. Kutolewa kwake kuliwapa nguvu wenyeji na dakika ya 85, Kumbulani Madziba aliyewachambua mabeki wa Yanga na kuuminya kiulaini langoni kuandika bao la pili. Yanga iliyowasimamisha viungo imara; Twite, Haruna Niyonzima na Ngassa, ilikosa mabao matatu ya wazi kipindi cha kwanza kupitia kwa Tambwe, Mrwanda na Ngassa huku wenyeji wakipata hasara dakika ya 20 baada ya beki wao Othusitse ‘Nakata’ Mpharithe kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Msuva. BDF ambayo walikuwa wakifaidi maumbo yao marefu, hususani kwenye mipira waliyokuwa wakitanguliziwa mawinga wafupi wa Yanga, walicheza mpira wa taratibu huku wakishindwa kuendana na mbwembwe za Yanga ambayo kocha wake Hans Pluijm alionyesha uzoefu wa kimataifa kwa kuwatuliza wachezaji wakacheza bila mchecheto. Yanga ambayo ilitumia bajeti ya Sh168 milioni kwenye mechi mbili, ile ya Dar es Salaam na ya jana, ilianzisha kikosi chenye watu wenye kasi ambacho kilisaidia mashambulizi ya kushtukiza kwa kuwatumia Msuva, Ngassa na Mrwanda. Yanga sasa itacheza mchezo wa raundi ya kwanza Machi 14 na mshindi wa mechi ya leo Jumamosi baina ya Sofapaka ya Kenya na Platinum ya Zimbabwe mchezo utakaochezwa mjini Harare. Katika mechi ya kwanza jijini Nairobi, Sofapaka inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, Sam Timbe ilifungwa mabao 2-1. Mechi hiyo itachezeshwa na Mbotswana, Tirelo Mositwane. Mashabiki Awali mashabiki zaidi ya 100 wa Yanga waliotoka Dar es Salaam na mikoa ya jirani walikwama kuingia Botswana kuangalia mechi hiyo baada ya kuzuiwa mpakani mwa Zambia kwa kuwa hati zao za kusafiria ni za karatasi. Kwa mujibu wa maofisa wa uhamiaji wa eneo hilo, pasi hizo haziruhusiwi bali zile za vitabu ndizo halali za kuingilia kwenye nchini hiyo. Chakula na Basi Chakula cha mchana wachezaji wa Yanga walikula kwenye hoteli tofauti na ile waliyofikia na wakati Yanga inaondoka pia hotelini kwenda uwanjani ilibadili basi ambapo lile lililokuwa limeandaliwa na wenyeji kwaajili ya kutumiwa na wachezaji likapandwa na mashabiki na wachezaji wakakodiwa basi jingine na uongozi. Pondamali aachwa Katika tukio ambalo liliibua maswali mengi, Yanga walipoondoka hotelini walimsahau kocha wao wa makipa, Juma Pondamali ambaye walilazimika kumkodia usafiri maalum ili awahi mchezo huo. Zawadi Yanga ikipenya kwenye mechi sita zilizobaki ina uhakika angalau wa dola 150,000(Sh267 milioni). MWANASPOTI.
Ijumaa, 27 Februari 2015
JESHI LA CHINA LAINGIA SUDAN KUSINI.
Uchina imesema kuwa kikosi chake kwa kwanza maalum cha kijeshi kilichojumuishwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa kimeanza shughuli zake nchini Sudan kusini. Katika kipindi cha majuma machache yajayo, jumla ya wachina mia saba watawasili nchini humo . Watakuwa na ndege zisizokua na rubani, vifaru na makombora. Uchina haijawahi kuwatuma maelfu ya walinda amani , lakini imekuwa zaidi ikitoa misaada kwa ajili ya amani. .
WANAOLALA SANA KUSHIKWA NA KIHARUSI.
Watu wanaolala kwa zaidi ya masaa manane kwa siku wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kiharusi,utafiti umesema lakini wataalam hawajua sababu yake. Utafiti uliofanywa kwa takriban watu 10,000 katika chuo kikuu cha Cambridge ulibaini kwamba wale wanaolala kwa takriban saa nane wana uwezekano mkubwa wa asilimia 46 kupata kiharusi. Watu wazima hupendelea kulala kati ya saa sita na tisa ili kupumzika vizuri,lakini kulala zaidi hushirikishwa na matatizo ya afya kama vile ugonjwa wa sukari pamoja na ule wa kunenepa kupitia kiasi. Hatahivyo haijabainika kutoka kwa utafiti huo iwapo kulala kwa zaidi ya saa nane huenda ndiko kunakosababisha matatizo hayo ambayo husababisha kiharusi ama iwapo ni miongoni mwa sababu za magonjwa yasiojulikana. Utafiti huo ulifanywa miongoni mwa watu walioko na kati ya miaka 42 na 81. Kitengo cha ugonjwa kiharusi Watafiti walichunguza mienendo yao ya kulala kwa kipindi cha miaka 10 ambapo watu 346 walipatwa na kiharusi. Baada ya kuangazia athari kama vile miaka na jinsia, watu waliosema wamekuwa wakilala kwa zaidi ya masaa manane walipatikana na hatari ya asilimia 46 kupatwa na ugonjwa huo. Wale walioweza kulala kwa chini ya masaa sita walipatikana na hatari ya asilimia 18.
MKONGA WA MAWASILIANO WATUA TPB.
BENKI ya Posta Tanzania (TPB) imedhamiria kuunganisha matawi yake yote katika mfumo wa kisasa wa Nyaya zitumikazo kuunganisha mawasilino.
BENKI ya Posta Tanzania (TPB) imedhamiria kuunganisha matawi yake yote katika mfumo wa kisasa wa mawasiliano kupitia mkongo wa mawasiliano nchini (Fiber Optic) ili kuboresha huduma na mawasiliano katika huduma zake. Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa alipokuwa akizungumza katika makabidhiano ya mradi mpya wa benki hiyo uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo mbalimmbali nchini. Tawa amesema mpaka sasa matawi ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Samora, Metropolitan, YWCA, Mkwepu, Ubungo na Kijitonyama tayari yameunganishwa kwenye mfumo huo mpya na wa kisasa kimawasiliano. "..Mpaka hivi sasa matawi yetu 11, yakiwemo Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Samora, Metropolitan, YWCA, Mkwepu, Ubungo, Kijitonyama, tayari zimeunganishwa kwenye mfumo huo. Hii ni katika hatua ya mwanzo tu ya mradi huu, kwani benki ya Posta imekusudia kuyaunganisa mtawi yake yote kwenye mfumo huu," amesema Tawa. Amesema baada ya kukamilisha matawi ya TPB katika mfumo wa Mkongo (Fiber Optic), imepata mafanikio makubwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo matawi haya yalikuwa yameunganishwa na mtandao wa teknolojia ya Copper (Copper network).
Aidha akizitaja faida ambazo benki hiyo imezipata baada ya kujiunga na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unaosimamiwa na kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ni pamoja kupungua kwa msongamano wa wateja kusubiria huduma kwenye matawi, kuongezeka kwa ufanisi na kupungua kwa dharura ya kusitisha huduma kwa muda. "...Pia tumeboresha uwezekano wa kutambua tatizo lolote linalotokana na kukatika kwa mawasiliano kwani huu ni mfumo wa kidijitali...kupungua kwa gharama za uendeshaji katika benki yetu." alisema Tawa. Kwa upande wao TTCL ikikabidhi mradi huo kwa TPB, Mtatuzi wa Masuala ya Kiufundi, Fredrick Bernard alisema mfumo huo wa mkongo unafaida kubwa kwani, mbali na kuwa salama zaidi pia unauwezo wa kugundua tatizo la mawasiliano kabla ya kutokea hivyo kufanyiwa kazi mapema. Amesema hata hivyo alisema njia za kupitisha mawasiliano hufanya kazi kwa kutegemeana na zipo zaidi ya moja hali ambayo huwezesha hata njia moja kuisaidia nyingine inapopata tatizo huku tatizo lililojitokeza likishughulikiwa kwa wakati huo. Faida hizo pamoja na nyingine nyingi zinaifanya benki ya Posta iamini kuwa huduma hii ya Mkongo itolewayo na TTCL ni bora nchini na itatusaidia sana sisi benki ya Posta kuboresha huduma zetu na kuongeza ufanisi katika shughuli zetu za kibenki.
MV DAR ES SALAAM YAANZA MAJARIBIO,YAENDA BAGAMOYO NA KURUDI DAR.
Di Maria ajuta kujiunga na Man United
Mwandishi wa Uhispania Manolete Esteban anadai kwamba mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya Real Madrid ambaye amekosolewa kwa uchezaji wake amewaambia marafiki zake kwamba anajuta kuondoka katika kilabu ya Real Madrid.
Esteban aliiambia runinga ya Uhispania katika kipindi cha La Goleada kwamba Di maria alikiri kwa rafikiye katika kilabu ya Real Madrid kuwa anajuta kujiunga na Manchester United.
Je rinda hili ni la rangi gani ?
''je ni la Dhahabu na Nyeupe ama ni leusi na samawati ''bluu''
Na kila aliyejaribu kuijibu alizidisha utata.
Mwanamziki Taylor Swift akapalia moto aliposema kuwa rinda hilo ni leusi na samawati(bluu)
“baada ya kutafiti rangi tofauti chuoni kwa miongo mitatu mwanachuoni Jay Neitz, wa chuo kikuu cha Washington kilichoko Seattle, marekani amesema utata huu unatokana na tofauti za genetiki.
Watu wenye umri mkubwa wanaupungufu wa uwezo wa kuona rangi ya samawati(bluu) kwa hivyo watasema kuwa rinda hilo ni leupe na dhahabu lakini kimsingi ni ulemavu wa macho , alisema Neitz.
Mwanachuoni huyo hata hivyo alitamatisha maoni yake kwa kusema kuwa rangi haswa ya rinda hilo inamtegemea saikolojia ya yule anayeitazama.
Kazi kwako msomaji je ni ya rangi gani rinda hili
Ujerumani yaridhia kuinusuru Ugiriki
baadhi ya Wabunge wa Ujerumani wameshuku kuhusu mpango huo ambao unaelezwa kuwa utaweza kupita kirahisi.
Hatua hii inakuja baada ya Polisi na Waandamanaji kupambana wakati wa Maandamano mjini Athens siku ya Alhamisi.
Hizi ni vurumai za kwanza tangu Chama cha Mrengo wa kushoto cha Ugiriki Syriza kuongoza Serikali kuu ya Ugiriki.
Wanaharakati waliwarushia mabomu ya Petroli na mawe Polisi na kuchoma moto magari baada ya Matembezi yaliyohusisha mamia ya Waandamanaji.
Mpango wa kupata mkopo pia umetikisa Chama cha Syriza.
Chinja chinja wa IS akamatwe:Ndugu
Bi.Dragana amesema tangu alipojua kuwa mmewe David amechinjwa alijipa matumaini moyoni mwake kuwa ipo siku muuaji huyo atafahamika na hatimaye kukamatwa.Lakini baada ya kupatika kwa taarifa hizi za muuaji huyo anasema kuwa itakuwa faraja ya pekee kwa familia za kila aliyeuawa kinyama na wauaji hao, kwa sababu kama atakutwa amekufa anaona hicho kitakuwa ni kifo cha heshima kwa Mohamed Emwazi, lakini maombi yake ni kwamba kukamatwa akiwa hai na afe baadaye.
Kwa upande wake Barak Barfi ambaye ni msemaji wa familia ya Sotloff iliyopoteza ndugu yao pia, anasema kuwa hawana wasiwasi juu ya kukamatwa kwake muuaji huyo Mohamed Emwazi ama JIHAD JOHN.
"Tuna Imani kubwa sana na nchi ambayo vyombo vyake vya usalama na kiintelijensia vitawakamata watu hawa.Tungependa kwenda kumuangalia muuaji huyu ana kwa ana wakati wa mashtaka yake katika mahakama ya Marekani,na pia kuona akitumikia kifungo chake, katika gereza maalumu ambako ataishi huko pekee yake katika upweke.hiyo ndiyo sheria ya Marekani na hivyo ndivyo nchi yetu inavyoshughulikia matatizo kama haya"amesema Barak
Sera ya Ardhi:Mugabe akiri kushindwa
Mwanzoni alilenga kutupa lawama kwa kilimo duni, hali ya hewa na Vikwazo kutoka nchi za magharibi.
Kunyang'anya ardhi kutoka kwa Wakulima weupe, kumeonekana sababu kubwa ya kudorora kwa uchumi wa Zimbabwe tangu mwaka 2000.
Mwandishi wa BBC mjini Harare amesema si mara ya kwanza kwa Mugabe kukosoa Wakulima weusi.
Mugabe, alitaka kuwahamasisha Wakulima kujihusisha na kilimo cha Ngano,amewalaumu kwa uzalishaji duni wa Wakulima wanaolima mazao ya Biashara pia kwa kushindwa kutumia ardhi yote.
''Utawaona Wakulima wengi wanatumia theluthi moja tu ya Shamba zima,'' Gazeti la Serikali ya Zimbabwe, Herald lilimnukuu Mugabe.
Jeshi la China laingia Sudan Kusini
Watakuwa na ndege zisizokua na rubani, vifaru na makombora.
Uchina haijawahi kuwatuma maelfu ya walinda amani , lakini imekuwa zaidi ikitoa misaada kwa ajili ya amani. .
BENSOUDA AWASILI UGANDA,KUNANI?
WATU 17 WAUAWA KWA BOMU NCHINI NIGERIA.
Wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wakidhoofisha hali ya usalama nchini Nigeria.
Takriban watu 17 wameuawa kwa Bomu la kujitoa muhanga katika kituo cha mabasi mjini Biu, huku mtu mwingine aliyekuwa na nia ya kujitoa muhanga ameripotiwa kukamatwa na Watu na kupigwa mpaka mauti yakamkuta. Mjini Jos, Watu 15 waliuawa kwa mabomu matatu yaliyorushwa kutoka kwenye Gari katia eneo la kituo cha mabasi na Chuo kikuu. Uchaguzi wa Urais mwezi Februari umeahirishwa kwa sababu ya machafuko. Uchaguzi sasa unatarajiwa kufanyika tarehe 28 mwezi March Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, ambaye alikuwa na ziara kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, mjini Baga, amesisitiza kuwa Jeshi linawakabili wanamgambo wa Boko Haram. Jeshi lilirudisha mji wa Baga kutoka mikononi mwa Boko Haram Wiki iliyopita .Kundi hilo bado linakabili sehemu kubwa ya Kaskazini Mashariki mwa jimbo la Borno na zaidi ya Watu milioni tatu wamekimbia makazi yao. Mashambulizi mjini Kano na Potiskum siku ya jumanne yaligharimu maisha ya Watu zaidi ya 50.Hakuna kundi lolote lililokiri kutekeleza mashambulizi hayo. BBC.
Alhamisi, 26 Februari 2015
UPANDIKIZAJI WA KICHWA SASA UNAWEZEKANA.
Upandikishaji wa kichwa cha binaadamu hadi katika mwili mwengine sasa unawezekana kulingana na wanasayansi Unaposikia habari hii utadhani ni maudhui ya filamu ya kutisha ,lakini wanasayansi wanaamini upasuaji wa upandikishaji wa kichwa cha mwanadamu katika mwili mwengine huenda ukafanikiwa. Madaktari watazindua mradi huo katika kongamano wakati wa msimu wa joto ,kwa lengo la kuanzisha utaratibu huo mnamo mwaka 2017. Mtu atakayeongoza mpango huo ni daktari raia wa Italy Sergio Canavero kutoka kundi moja la wanasayansi mjini Turin. Anaamini kwamba upandikishaji wa vichwa vya watu utawasaidia wanaosumbuliwa na magonjwa ya misuli na saratani. Baada ya kutoa wazo hilo mnamo mwaka 2013,daktari Canavero anaamini vikwazo vikuu vya upasuaji huo vimekabiliwa ,kulingana na ripoti mpya ya wanasayansi. Vikwazo hivyo ni pamoja na usimamizi wa uti wa mgongo kuingiliana na kichwa kipya pamoja na kuhakikisha kuwa kinga ya mwili haikikatai kiungo hicho kipya. Daktari Canevaro alichapisha taarifa iliokuwa na nadharia kuhusu vile anavyoamini upasuaji huo unaweza kufanyika.
MCHINJAJI WA IS 'JIHADI JOHN' ATAMBULIWA.
Mwanaume ambaye amekuwa akitekeleza mauaji ya mateka wa kundi la wapiganaji wa Islamic State ajulikanaye kwa jina la utani "Jihadi John",ametambuliwa. Mwanaume ambaye amekuwa akitekeleza mauaji ya mateka wa kundi la wapiganaji wa Islamic State ajulikanaye kwa jina la utani "Jihadi John",ametambuliwa. Bwana huyo ambaye taswira yake akiwachinja mateka kwa kisu bila huruma ndiyo nembo ya wapiganaji hao sasa ametambuliwa kuwa anatokea Uingereza. Shirika la Habari la BBC limetambua kuwa jina lake kamili ni Mohammed Emwazi. Emnuazi ameonekana kwenye video kadhaa ya mauwaji ya mateka wa mataifa wa magharibi, akiwemo Mmarekani James Foley, Raia wa Uingereza, Alan Henning na mwaandishi habari wa Japan, Kenji Goto. Inaaminika kuwa Emwazi ni raia wa Uingereza na hasa anatokea magharibi mwa London. Yamkini Emnuazi aliyezaliwa Kuwaiti na mwenye umri wa kati ya miaka 20 -29 alikuwa amefahamika sana na vyombo vya usalama lakini kwa sababu za kiusalama haikuwezekana kumtambua. Anaaminika amewahi kuishi Somalia mnamo mwaka 2006 na anauhusiano mkubwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabab nchini humo. Polisi nchini Uingereza imeziomba vyombo vya habari kutosambaza habari ambazo hawajazithibitisha kumhusu jamaa huyo kwani uchunguzi unaendelea. Hata hivyo bado habari za kina kumhusu Jihadi John hazijatolewa. Mwandishi wa maswala ya Usalama wa BBC Tomi Oladipo anasema kuwa vyombo vya usalama vya serikali za mataifa yanayokaribia Somalia sasa yana kila sababu ya kutahamaki. Bwana huyo aliwahi kushirikiana na kundi la Al Shaabab Kwa sababu Kuhusika kwake na kundi la Al Shaabab kisha akajiunga na kundi la Islamic State ambalo kwa wakati mmoja lilikuwa linashindana na wanamgambo wa Al Qaeda kuhusu yupi kati yao anayeushawishi mkubwa Ishara kuwa Al Shabab inazingatia msimamo mkali wa kidni hata zaidi ya Al Qaeda. Kwa sababu itakumbukwa kuwa Al Qaeda ilipinga hatua kali ya kuwachinja mateka nchini Iraq na Syria. Emnuazi ambaye amekuwa akiwabeza mataifa ya Magharibi kabla ya kuwakata shingo naaminika kuwa mtaalamu wa maswala ya kompyuta alisomea chuo kikuu cha Westminster. Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC bwana huyo anaaminika kuwa alikwenda Syria mwaka wa 2012, lakini kabla ya wakati huo majasusi wa Uingereza na Marekani walikuwa hawajajua tishio lake. BBC.
MFANYAKAZI WA MUDA MREFU POSTA AFARIKI.
Mfanyakazi wa muda mrefu wa shirika la posta,Mzee Nyalima amefariki dunia leo wilayani Nachingwea.
Taarifa kwa ufupi zilizoifikia blog hii ni kwamba mzee amefariki leo katika hospitali ya wilaya lakini chanzo cha kifo chake bado hakijatufikia .
Mzee mpaka anafariki dunia bado alikuwa mfanyakazi wa posta.
ENZI ZA UHAI WAKE.
Enzi za uhai wake,mzee Nyalima alikuwa mchapakazi hodari kwani zama hizo,alisema walitumia usafiri wa miguu na baiskeli wakati mwingine kusambaza barua na vifurushi vingine kutoka wilaya moja kwenda nyingine.Hizo zilikuwa kati ya changamoto alizokutananazo akiwa kazini tofauti kabisa na zama hizi za sayansi na teknolojia.
Naipa pole familia ya marehemu na kuitakia roho ya uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU PEPONI....AMINA.
WAKRISTO ZAIDI WATEKWA NYARA SYRIA.
EBOLA:MFANYAKAZI APOTEZA MAISHA.
Raia mmoja wa Sierra Leone aliyekuwa akiwatunza Watoto walioachwa yatima kutokana na ugonjwa wa Ebola amekufa kutokana na ugonjwa huo. Augustine Baker alifikishwa katika kituo cha matibabu baada ya kuugua juma lililopita. Baker alikuwa akifanya kazi katika Kituo cha Watoto yatima kinachoendeshwa na kituo cha msaada kutoka Uingereza.Kituo hicho kiko nje ya mji wa Freetown. Watoto 33 na Wafanyakazi saba katika nyumba ya yatima St George, wamewekwa katika Karantini tangu Bwana Baker alipobainika kuwa na Virusi vya Ebola. Kituo hiki kilianzishwa mwaka 2004 mpaka pale Ugonjwa wa Ebola ulipoingia, kituo kilijikita zaidi katika kuwaokoa Watoto wa mitaani. Mwaka jana kituo kiliwasaidia Watoto takriban 200 walioachwa na familia kutokana na Ebola. Ebola imeua zaidi ya Watu 9,500 nchini humo,Liberia na Guinea. Lakini katika kipindi cha majuma ya hivi karibuni, kasi ya maambukizi ya Ugonjwa huu imepungua na Serikali za nchi tatu zimeahidi kumaliza kabisa tatizo hili ndani ya miezi miwili ijayo. BBC.
Jumatano, 25 Februari 2015
WAFUASI WATATU WA IS,WAKAMATWA MAREKANI.
DAWA YA KUPAKA ILI KUZUIA HIV HAIFAI.
Dawa za ugonjwa wa ukimwi Dawa iliokisiwa kupunguza uwezekano wa mwanamke kupata virusi vya HIV wakati wa tendo la ngono haifai,kulingana na utafiti mkubwa uliofanywa na shirika la Follow on Africa Consortium for Tenofovir kutoka Afrika kusini. Matokeo ya utafiti huo unaojulikana kama facts 001 yalitolewa katika kongamano la magonjwa ya virusi na yale ya maambukizi nchini Marekani. Kulingana na gazeti la mail and Guardian nchini Afrika kusini,wanawake katika utafti huo waliagizwa kujipaka dawa hiyo katika sehemu zao za siri kabla na kila baada ya tendo la ngono. Matokeo hayo yanapinga matokeo ya utafiti mwengine uliochapishwa mwaka 2010 na shirika la mpango wa utafiti wa ugonjwa wa ukimwi nchini Afrika kusini Caprisa. Watafiti waliwatumia zaidi ya wanawake 900 katika jimbo la Kwa Zulu Natal na kuripoti dawa hiyo ya Tenofivir ilikuwa na uwezo wa asilimia 39 pekee wa kupunguza viwango vya maambukizi ya viini vya HIV miongoni mwa wanawake hao. Viwango vya maambukizi ya HIV nchini Afrika kusini vilikuwa asilimia 12.2 mwaka 2012 ikiwa ni vya juu zaidi duniani kulingana na utafiti wa baraza la sayansi ya binaadamu kuhusu kinga ya HIV ,visa na tabia. Viwango hiyo ni vya juu miongoni mwa wanawake na kusababisha utafiti kutafuta tiba za kinga zinazowalenga wanawake kama vile dawa inayopakwa katika sehemu za siri,pamoja na sindano zilizojaa tiba za kukabiliana na HIV. Wakati wa utafiti huo uliochukua takriban miaka mitatu,watafiti waliwatumia wanawake 2000 wasio na virusi vya ukimwi kati ya miaka 18 hadi 30, na kuwapatia nusu yao dawa ya Placebo na nusu nyengine wakapewa dawa ya kwenye sehemu za siri tenofivir,ambayo ni dawa ya kukabiliana na virusi vya ukimwi. Baadaye watafiti walipima viwango vya maabumizi ya virusi vya HIV kati ya makundi mawili na kubaini kwamba wanawake waliopewa dawa hiyo ya Tenofivir waliambukizwa virusi vya ukimwi sambamba na wanawake waliopewa dawa kupaka ya placebo. Kwa jumla wanawake 123 waliambukizwa virusi vya HIV huku 61 wakiwa ni wale waliopewa mafuta ya Tenofivir na 62 wakiwa walipewa mafuta ya placebo. BBC.
UANDIKISHWAJI KWA ELEKTRONIKI UMESHINDWA?
Teknolojia mpya inaelezwa kukumbwa na changamoto inayokwamisha zoezi la uandikishaji kufanyika kwa ufanisi Vyama vya upinzani nchini Tanzania vimeendelea kuishinikiza serikali kuachana na mpango wa kura ya maoni juu ya katiba inayopendekezwa na badala yake itatue changamoto zinazojitokeza wakati wa kuandika wapiga kura kwa kutumia mitambo ya BVR ili iweze kukamilika kwa ufanisi. CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI na NLD kupitia uongozi wao vimesema serikali inatakiwa kusikiliza malalamiko yanayotolewa juu ya namna mfumo wa uandikishaji unaoendelea ili kazi hiyo isikwamishe uchaguzi uchaguzi mkuu. Moja ya changamoto zinazozungumziwa ni pamoja na idadi ndogo ya mashine hizo kuweza kumudu idadi ya wale wanaotakiwa kuandikishwa. Awali, mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi alieleza BBC kuwa mpaka zoezi linaanza zilikuwepo mashine 250 tu kati ya 8000 zinazohitajika lakini akadai 7,750 zilizosalia serikali ilikuwa imeshazilipia na zinategemewa kufika nchini wiki ya kwanza ya mwezi wa tatu. "Habari tulizo nazo siyo hata mashine zote zinafanya kazi hi sasa huko Njombe, bali ni mashine 82 tu huku nyingine zikiwa zimepelekwa kufundishia watakaoandikisha katika mikoa mingine" Amesema Freeman Mbowe Mwenyekiti wa chama kiii cha upinzani CHADEMA. Vile vile kutokana na mashine hizo kuwa na sehemu iliyotengenezwa na bati katika eneo lake la chini zilikuwa zinapata joto, hata hivyoTume inasema changamoto hiyo imetatuliwa. Kasoro nyingine iliyojitokeza ni mashine hizo kushindwa kutambua alama za vidole vya baadhi ya watu ambao ngozi zao za vidole zina michubuko. Aidha, mashine hizo zimekuwa zikitumia muda mwingi kuhifadhi taarifa za mtu mmoja jambo ambalo linaleta hofu iwapo kazi hiyo itakamilika mapema na kwa ufanisi. Lengo la kuandika wapiga kura kwa njia ya mitambo ya BVR ni kuboresha daftari la wapiga kura ambalo lilikuwa linalalamikiwa na vyama vya siasa kuwa lina upungufu mwingi ikiwamo uwezekano wa kumruhusu mtu kupiga kura zaidi ya mara moja. Iwapo kazi hii itakamilika, kumbukumbuku zitakazohifadhiwa na mitambo hiyo zitatumika mwezi aprili wakati wa kupiga kura ya maoni ya kuamua iwapo Katiba mpya inayopendekezwa inafaa au la na baadae katika uchaguzi mkuu uanaotarajiwa mwezi oktoba mwaka huu. BBC.
HALMASHAURI YA MASASI YAPUNGUZA KIASI CHA FEDHA KUTOKA MIRADI MINGINE ILI KUKARABATI BWAWA LA NANJOTA.
FAIDA ZA TUNDA LA CHUNGWA.
Katika utafiti wa hivi karibuni uliofanywa kwenye tunda la chungwa, iligundulika kwamba tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuponya matatizo mbalimbali ya kiafya kwa sababu lina mkusanyiko mkubwa wa virutubisho vya Phytonutrients. Jamii ya virutubisho hivyo inajumuisha pamoja na citrus flavanones, anthocyanins, hydroxycinnamic acids na polyphenols, ambapo inaelezwa kwamba virutubisho hivyo vinapochanganyika na Vitamin C inayopatikana kwenye chungwa, uwezo wake wa kutoka kinga mwilini huwa mkubwa. Moja ya faida nyingi za virutubisho hivyo ni pamoja na kushusha kiwango cha shinikizo la damu pamoja na kiwango cha mafuta mabaya mwilini, maarufu kwa jina la Kolestro. Jambo la muhimu kuzingatia sana hapa ni kwamba virutubisho vingi muhimu vinapatikana kwenye maganda na nyama nyeupe ya chungwa na siyo kwenye maji peke yake. Kwa maana nyingine ili upate vitamini na virutubisho vyote muhimu vinavyopatikana kwenye tunda la chungwa, inashauriwa kulila pamoja na nyama zake, na siyo kukamua maji peke yake. Ingawa wa kufanya hivyo bado una uhakika wa kupata Vitamin C ambayo ndiyo inapatikana kwa wingi kwa kunywa juisi yake tu.
UNAUJUA UMUHIMU WA VITAMIN C ?
Bila shaka utakuwa unaelewa tangu zamani kwamba chungwa ni chanzo kikubwa cha Vitamni C, kwani chungwa moja lina uwezo wa kutoa hadi asilimia 116 ya kiwango kinachotakiwa kwa siku, lakini pamoja na kujua hilo, unafahamu Vitamini C na machungwa kwa ujumla ni muhimu kiasi gani katika afya yako? Kwanza kabisa Vitamini C hutoa kinga ya mwili kupambana na maradhi kama vile mafua, kikohozi na hata kifua kikuu na vile vile huondoa vijidudu nyemelezi (free radicals) mwilini na kuzipa seli kinga madhubuti ya kutoharibika, nje na ndani. Inaelezwa kwamba hatari kubwa ya kwanza seli inapokuwa haina kinga dhidi ya vijidudu nyemelezi, ni kupatwa na saratani, hasa ya utumbo. Lakini ukiwa na Vitamni C ya kutosha mwilini, unakuwa umejitengenezea kinga madhubuti dhidi ya saratani hiyo. Aidha seli zinapokuwa zimedhurika kwa kukosa kinga, mwili mzima huwaka moto kwa maumivu, hasa wakati mwili unapokuwa ukijaribu kuondoa seli zilizodhurika. Hivyo inaelezwa kwamba Vitamin C, ambayo ndiyo huzuia vijidudu nyemelezi vinavyosababisha maumivu ya mwili kuongozeka, hutoa nafuu zaidi kwa magonjwa hayo na mengine kama pumu na viungo. Vilevile vijidudu nyemelezi (free radicals) ndivyo vinavyosababisha kuganda kwa kolestro mwilini ambapo inapofikia hali hiyo husababisha kuziba kwa mishipa ya damu na mwisho huleta mshituko wa moyo au kiharusi. Lakini kwa mwili kuwa na Vitamin C ya kutosha, hali hiyo haiwezi kutokea kwani Vitamin hii ina uwezo wa kudhoofisha vijidudu hivyo visilete uharibifu.
GLASI MOJA YA JUISI NI BORA KULIKO VIDONGE
Utumiaji wa vidonge vya Vitamin C hauwezi kutoa faida za kinga sawa kama kunywa glasi moja ya juisi halisi ya machungwa, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kitengo cha Virutubisho vya Binadamu cha Chuo Kiuu cha mjini Milan, Italia. Hii ina maana kwamba ukinywa juisi halisi ya machungwa utapata faida za kinga zaidi kuliko kula vidonge vyake (food supplements). Kwa kutambua faida za kiafya zinazopatikana kwenye Vitamin C, si jambo la kushangaza kuambiwa na watafiti wetu kwamba ulaji wa matunda na mboga zenye kirutubisho hicho kwa wingi, vina uhusiano mkubwa wa kupungua, kwa kiasi kikubwa, kwa vifo vitokanavyo na ugonjwa wa moyo, kiharusi na saratani. (Heart Disease, stroke and cancer).
CHUNGWA CHANZO KIZURI CHA 'FIBER'
Faida za kiafya za chungwa zingali zikiendelea hadi kwenye kirutubisho kingine kinachojulikana kama 'fiber' au ufumwele. Tunaelezwa kwamba chungwa moja tu hutoa asilimia 12.5 ya kiwango cha ufumwele kinachotakiwa kwa siku katika mwili wa binadamu, kirutubisho hiki kimeonesha uwezo mkubwa wa kupunguza mafuta mabaya mwilini (cholestro). Vile vile ufumwele unasifika kwa kudhibiti kiwango cha sukari mwilini, hivyo chungwa ni tunda muhimu kwa wangonjwa wa kisukari, hasa wanapokula pamoja na nyama yake. Kwa kuongezea, sukari ya asili inayopatikana kwenye chungwa (fructose), inaweza kusaidia kudhibiti kupanda kwa kiwango cha sukari mara baada ya mgonjwa kula chakula. Vile vile ufumwele unaopatikana kwenye chungwa una uwezo wa kuondoa viwakilishi vinavyosababisha saratani ya utumbo kwa kutoa utandu wa kinga kwenye tumbo. Mbali na hilo, machungwa pia hutoa nafuu kwa watu wanaosumbuliwa na tumbo au ugonjwa wa kuharisha. Kula chungwa na nyama yake ili upate faida zote zinazopatikana kwenye virutubisho vilivyomo kwenye tunda hilo.
CHUNGWA HUONDOA MAWE KWENYE FIGO (Kidney stones).
Kama unataka kujikinga na ugonjwa wa kupatwa na mawe kwenye figo, basi unashauriwa kunywa juisi ya machungwa! utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa kwenye jarida la masuala ya lishe la Uingereza (British Journal of Nutrition), uligdundua kwamba wanawake walipokunywa nusu lita mpaka lita moja ya juisi ya machungwa au zabibu kila siku, usafishaji wa njia ya mkojo uliongezeka hivyo kuondoa kabisa hatari ya kuwa na mawe kwenye figo (calcium oxalate stones).
CHUNGWA HUTOA KINGA DHIDI YA VIDONDA VYA TUMBO.
Chungwa moja kwa siku, linaweza kukusaidia kukupa kinga dhidi ya vidonda vya tumbo, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa kwenye jarida la Chuo cha Lishe cha nchini Marekani ambapo zaidi ya watu wazima 6000 walifanyiwa utafiti kuthibitisha hilo. HITIMISHO Kwa ujumla, hizo ni faida chache tu na muhimu zinazopatikana kwenye tunda hili, lakini kuna faida nyingine nyingi tu. Kimsingi tunashauriwa kula matunda ya aina mbalimbali kwa wingi kadri tuwezavyo, kwani kwa kufanya hivyo tutajihakikishia upatikanaji wa faida zote za kiafya zilizomo kwenye matunda. Kwa kula matunda mengi na mchanganyiko, ndiko kunakoweza kukupa kinga ya mwili na afya njema iliyohuru na maradhi sugu kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu, kiharusi, kisukari, n.k. Mungu ametupa matunda mchanganyiko yanayopatikana mwaka mzima katika vipindi tofauti, kwa sababu maalum. Hivyo ni kosa kubwa sana kuacha kutumia matunda haya ya msimu kila yanapopatikana na ni makosa makubwa kiafya kujenga tabia ya kutokula tunda la aina yoyote hata kwa mwaka mzima. Kuanzia leo anza kulithamini chungwa na kuliona kama mkombozi wa afya yako.
Jumanne, 24 Februari 2015
MAJESHI YA DRC YASHAMBULIA NGOME YA FDLR.
Vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo FARDC, vimeanzisha hatua za kijeshi dhidi ya waasi wa Rwanda wa kundi la FDLR, Jumanne hii Tangu asubuhi mapema kumeripotia shughuli za kijeshi katika vijiji vya Ruvuye na Mulindi katika misitu ya maeneo ya mji wa Lemera tarafani Uvira mkoani Kivu ya kusini . Baadhi wa wajumbe wa kundi hilo wanashutumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda kabla ya kutoroka katika nchi jirani ya Jammuhuri ya kidemokrasi ya Congo, ambako pia wanashutumiwa kutekeleza ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, yakiwemo mauaji, ubakaji na uporaji. Mwandishi wa BBC wa mashariki mwa Kongo Byobe Malenga alituandalia taarifa ifuatayo. Silaha nzito nzito pamoja na bunduki za rashasha zimesikika hii leo tangu asubuhi mapema katika vijiji vya Ruvuye na Mulindi katika misitu ya maeneo ya mji wa Lemera tarafani Uvira mkoani Kivu ya kusini . Vyanzo vya idara ya 33 ya wanajeshi wa Mkoa zinaonyesha kuwa hatua hio nialama ya kuanza rasmi shughuli za kijeshi dhidi ya waasi hao wa kihutu toka Rwanda wa FDLR katika mkoa wa Kivu ya Kusini,huku vikisema kua askari wa taifa FARDC,wamedhibiti kambi ya Revo kutoka mikono mwa waasi hao kilomita thalathini na mji wa Lemera . Kamanda wa harakati hizo maarufu "Sukola 2" dhidi ya wapiganaji wa Rwanda FDLR katika Kivu ya Kusini, Generali Esperant Masudi, yupo kwenye eneo la mapambano katika misitu ya Lemera ajili ya shughuli hizo. Jeshi la Congo Kupitia Generali Didier Etumba, lilitangaza Januari 29 kama mwanzo wa operesheni dhidi ya waasi wa FDLR. Lakini mapigano yalikuwa bado kuaanza katika maeneo yote ya hapa nchini. Raia wa hapa mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo wameonyesha mtazamo wao kuhusiana na hatua hio ya jeshi la Congo FARDC kuanzisha mashambulizi dhidi ya waasi hao. Wapiganaji wa FDLR FDLR wanapatikana sio tu katika mkoa wa Kivu Kusini bali katika maeneo mbalimbali ya ya mashariki mwa hapa nchini kwa zaidi ya miaka ishirini sasa huku wakituhumiwa kwa vitendo vya ualifu. Hata hivyo, vikosi vya jeshi la DRC FARDC vinaendesha shughuli hizo peke yake, bila msaada wa vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa MONUSCO. Umoja wa Mataifa ulisitisha msaada wake kwa jeshi la Congo kwa kile walichokisema kuwepo wa majenerali wawili ndani ya operesheni hizo ambao wanatuhumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu . kutokana na utata uliopo katika mawasiliano ya pande hizo mbili,hatua hio ilipelekea serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kukataa msaada wowote kutoka kwa vikosi vya umoja wa mataifa MONUSCO katika operesheni hizo dhidi ya waasi wa Rwanda wa FDLR. Rais Joseph Kabila, alitoa kauli hiyo katika hotuba kwa mabalozi mjini Kinshasa. BBC.
Je wewe huoga mara ngapi kwa siku?
Utafiti uliofanywa nchini Uingereza kukagua ngozi za wanawake 2,021 wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 50 umegundua kuwa mbili ya tatu ya wanawake wana tabia ya kutoosha nyuso zao zenye poda kabla ya kulala na moja ya nane ya wanawake pia huwa hawana utamaduni wa kupiga mswaki kabla ya kulala.
Linapokuja suala la kuoga asubuhi sasa,ni asilia ishirini na moja tu ya wanawake ambao hutenga muda wa kuoga asubuhi kila siku,na asilimia thelathini na tatu ya wanawake huishi kwa siku tatu bila ya kukutana na maji mwillini mwao.
Jambo la kushangaza mmoja kati ya wanawake watatu huthubutu kukaa kwa siku tatu bila ya kuosha nyuso zao pia, kama utashangaa juu ya miili isiyooshwa kwa siku tatu.
Pamoja na kwamba wataalamu wa masuala ya fya na usafi wa kawaida wa mwili, asilimia hamsini na saba ya wanawake wa Uingereza wanakiri kutumia karatasi laini zenye maji maji kujifuta mwilini kabla ya kulala.
Utafiti uliofanywa uliwafikia wanawake elfu mbili,inaelezwa kuwa asilimia tisini na mbili wamesema wazi kuwa wanaelewa umuhimu wa utunzaji ngozi,lakini mtindo wa maisha huwanyima usingizi na ukosefu wa maji mwilini na hivyo kujiletea madhara kiafya na hasa ngozi zao.
HUWA UNAOGA MARA NGAPI?
Kila siku? Baada ya siku moja? Mara mbili kwa wiki,mara moja kwa mwezi? Iwe nataka ama lah,utafiti ukaeleza kuwa asilimia themanini na tisa ya wanawake wanajitetea kuwa wangependa sana kusafisha miili yao lakini uchovu wa asubuhi na jioni ndio sababu ya kutooga.
Mmiliki wa kampuni ya afya ya Flint + Flint Maxine Flint ansema kwamba anaelewa kuwa wanaojitetea wanadanganya, na kutooga hasa asubuhi haikubaliki kijamii, kwa watu wanaotuzunguuka na sio afya.
Anasema tunazungumzia dakika chache unazitumia kuoga kwa siku nzima,inaeleweka kuwa maisha ya sasa ni haraka haraka lakini kila mmoja pale alipo sio kweli kwamba hata muda wa kuoga tunaukosa, hatujatingwa kihiivyo.
Kwa muujibu wa taratibu za afya Maxine anasema ni vyema kusafisha nyuso zetu kila subuhi na kuukanda kwa joto ili kuchelewesha uzee usoni.Zaidi ya hayo ,idadi kubwa ya wanawake wanaelewa umuhimu wa utunzaji ngozi lakini bado hawazitunzi.
Roboti yahudhuria masomo kama mwanafunzi
Pennsylvania ilikodisha kifaa hicho kutoka katika kampuni inayotoa mafunzo ya namna ya kutumia roboti hizo katika mitandao ya kijamii.Kimsingi kifaa hicho ni sawa na iPad ambayo imeinuliwa juu vya kutosha.Naye Cole huwa anakiendesha kifaa hicho kupitia kinakilishi chake na vitufe vya kubofyea kitu ambacho yeye anakielezea kuwa sawa na kifaa cha michezo ya kinakilishi ya runinga.ana sema Roboti hiyo inamsaidia kufuatilia masomo yake bila taabu yoyote na pia awapo shuleni anakutana na marafiki zake .
Ni vyema na furaha kubwa kuonana na kila mmoja niliye mzoea na kuzungumza nao.
Wakuu wa shule anakosoma Cole wanasema roboti hiyo inawasaidia kupunguza gharama za mwanafunzi huyo.na wanajaribu kuzungumza kuwa hawajui ingekuwaje kwa mwanafunzi huyo bila kifaa hicho,pengine ingewalazimu kumpeleka mwalimu kila siku nyumbani kwa akina Cole kumfundisha,lakini roboti hiyo inamsaidia Cole kupata elimu bora,kwa kumpa maelekezo kupitia waalimu wake kama kawaida na roboti hiyo imekuwa sehemu ya darasa la Cole.
Kwa muujibu wa maelezo ya Cole, roboti hiyo si sanifu sana lakini si haba ni mwanzo mzuri na maendeleo yako wazi mbele yake.
Mahakama yaharamisha sheria ya Usalama Kenya
Jopo la majaji watano wa mahakama kuu wakiongozwa na Jaji Isaac Lenaola waliharamisha vipengee 10 kikiwemo kile kinachohusu uhuru wa vyomo vya habari na haki ya washukiwa wanapofikishwa mahakamani.
Uamuzi huo ulichukua takriban saa tano na majaji wakaamua kuwa baadhi ya vipengele havikuaambatana na katiba.
Katika uamuzi wao walikubali kuwa Kenya imekumbwa na visa vingi vya ugaidi katika miaka mitatu iliyopita na inastahili kuwa na mbinu za kuisaidia kukabilana na tatizo hilo…
hata hivyo majaji walisema kuwa haki za washukiwa zinatakiwa kuzingatiwa.
Mengine yaliyoharamishwa yanajumuisha kuwalazimisha wanahabari kuchapisha baadhi ya picha ya ruhusa ya polisi,
kuwazuilia washukiwa bila kuwapa nafasi ya kujitetea na kuwanyima dhamana washukiwa wakipelekwa mahakamani bila sababu za kuridhisha.
Aidha mahakama imeharamisha jaribio la serikali kutaka kuweka kiwango cha wakimbiai wanaotahili kuhifadhiwa Kenya kutozidi laki moja na nusu na kusema kuwa ni kinyume cha mkataba wa Geneva.
Ni uamuzi uliofurahiwa na muungano wa upinzani CORD.
Sheria hiyo tata ilipitishwa bungeni tarehe 14 Desemba mwaka uliopita katika kikao kilichokumbwa na vurumai huku wabunge wakipigana hadharani.
Baada ya hapo Rais Uhuru Kenyatta alitia saini mswada huo na kuufanya sheria tarehe 22 mwezi huo kisha chama cha CORD kikakwenda mahakamani kikidai kuwa sehemu nyingi za sheria hiyo zilikiuka katiba.
Mashirika mengine yalijiunga katika mchakato huo na kujumuishwa katika kesi ikiwemo tume ya kitaifa ya kutetea haki za binadamu.
Awali jaji wa mahakama kuu alikuwa amezuia vipengele vinane vya sheria hiyo kutotekelezwa na kumchochea mkuu wa sheria kukataa rufaa lakini bado mahakama ya rufaa ikashikilia uamuzi wa mahakama kuu.
Kinachosubiriwa kwa sasa ni kutazama mwelekeo utakaochukuliwa kwa misingi kuwa CORD inasema itaenda kwa mahakama ya rufaa vile vile kutaka sehemu nyingine za sheria hizo kuchunguzwa.
Nyaraka za siri zamuumbua,Netanyahu
Machafuko Ukraine yatazusha vita:Putin
Akizungumza kupitia televisheni Putin amesisitiza kuzingatiwa kwa mpango wa Amani ya mashariki mwa Ukraine uliojadiliwa Minsk na kupitishwa na baraza la usalama la umoja wa mataifa
Hata hivyo kwa mara nyingine Rais Putin amekanusha madai ya majeshi yake kushiriki katika mzozo.
Kiongozi huyo pia ameyaraja mataifa ya Urusi, ujerumani na Ufaransa kuma washirka mhimu katika utatuzi wa mgogoro huo na kwamba kupitia makubaliano ya Minsk pekee ndiyo itakuwa njia pekee ya kurejesha Amani ya Ukraine.
Kuhusiana na kutuhumiwa kwa taifa lake kuhusika katika mzozo huo Putin amesema wakati mwingine anashtushwa na kauli zinazotolewa na viongozi wa Ukraine dhidi ya Urusi,mfano tuhuma kuwa mamlaka za Urusi zilihusika na machafuko ya viunga vya Maidan mwaka mmoja uliopita.
Wasichana London wajiunga na IS Syria
Inaelezwa kuwa wanafunzi hao walipanda ndege ya shirika la ndege la Uturuki kutoka Uingereza na walihitaji hati ya kusafiri na visa kuingia Uturuki. Sakata la wanafunzi hao wa kike kutoka London kwenda kujiunga na wapiganaji wa Islamic State limekuwa limeshtua wengi.
Huku serikali ya Uturuki inasema ingechukua hatua kama ingepewa taarifa mapema Naibu Waziri Mkuu wa Bulent Arinc anatupa lawama moja kwa moja kwa Uingereza kwamba iliichelewa kuijulisha nchi hiyo kabla ya wanafunzi hao hawajaingia katika mji mkuu wa Instanbul.
"Tumefuatilia na tumezuia watu wapatao elfu kumi ambao hapo awali waliripotiwa kwetu kutaka kuingia Uturuki kwa tuhuma za kutaka kuendesha shughuli za kigaidi. Tumetimiza wajibu wetu. Kama Serikali ya Uingiereza ingetujulisha mapema maafisa wetu wa usalama wangechukua hatua madhubuti. Tunaamini kuna haja ya kuanganisha nguvu kwa pamoja ili kuratibu na kupambana na ugaidi." Alisema.
Wakati kukiwa na taarifa hizo za wanafunzi wa kike waliokuwa wakisoma London Uingereza kuingia nchini Syria kujiunga na Islamic State
Nayo serikali ya Ufaransa kwa mara ya kwanza imezikamata hati za kusafiria za raia wapatao sita ambao wanatuhumiwa kwenda nchini Syria kujiunga na wapiganaji hao wa Islamic State.
Waziri wa Mambo ya ndani wa ufaransa Benard Cazeneuve amesema kitengo cha ujasusi kinaamini kwamba watu hao walikuwa na mpango wa kusafiri na kwamba swala hilo linahusiana na mambo ya usalama.
"Tunaamini hatua hizi zilizochukuliwa zimefanikiwa kwa sababu kama raia wa Ufaransa watakwenda kupigana Iraq na Syria watasababisha hatari kubwa kwa usalama wa taifa wakati watakaporudi. Wanaweza kuendesha vitendo vya kigaidi kwa kiwango kikubwa." Alisema.
Jumatatu, 23 Februari 2015
CCM Serengeti wamtaka Mh Lowassa
Miaka 2 jela kwa kuigiza ufalme Thailand
Mahakama nchini Thailand imewahukumu wanafunzi wawili kifungo cha miaka miwili na nusu jela kila mmoja kwa kucheza mchezo uliotajwa kuwa uliuchafulia sifa ufalme .
Pornthip Munkhong na Patiwat Saraiyaem ni miongoni mwa wanafunzi walioandaa mchezo wa kuigiza ulioitwa mke wa mbwa mwitu Fisi yaani wolf's bride, katika chuo moja kikuu mjini Bangkok mwaka wa 2013.
Mchezo huo uliotumiwa kusherehekea ushindi wa wanafunzi wa kupinga utawala wa kijeshi miaka 40 iliyopita na haukuwa na ushawishi mkubwa nje ya chuo kikuu.
Lakini baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka uliopita, wakuu wa jeshi walishinikiza hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote au kundi lolote ambalo linakejeli ya kutusi utawala wa kifalme nchini humo, na hapo ndipo
wanafunzi hao walipokamatwa.
Wawili hao walikiri mashtaka dhidi yao ili kupata huruma ya kushawishi mahakama hiyo kupunguza hukumu yao,kwa kuwa ni vigumu sana kwa washtakiwa kushinda kesi kama hiyo na mara nyingi adhabu yake huwa kifungo cha
kati ya miaka kumi na ishirini gerezani.
Wanafunzi hao wanaamini kuwa wao hawakuwa na kosa lolote.
Mchezo huo uliangazia mfalme mmoja wa kudhaniwa aliyekuwa na chongo sawa na ya mfalme Bhumibol Adulyadej,ambaye alipoteza jicho lake moja akiwa mchanga, na kwa kufananisha hilo wakajiweka katika hatari ya
kufunguliwa mashtaka.
Jaji aliyesikiliza kesi hiyo alisema kuwa anafahamu kuwa washtakiwa walikuwa vijana wenye umri mdogo lakini walikuwa wamedunisha hadhi ya ufalme wa nchi hiyo, kitendo ambacho kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo adhabu
yake huwa kifungo gerezani.