Uturuki imeshutumu Uingereza kwamba imechukua muda mrefu kuijulisha nchi hiyo kuhusu wanafunzi wa kike watatu waliokuwa wakisoma London Uinger kwamba walisafiri kwenda nchini Syria kwa lengo la kujiunga na Islamic State.
Inaelezwa kuwa wanafunzi hao walipanda ndege ya shirika la ndege la Uturuki kutoka Uingereza na walihitaji hati ya kusafiri na visa kuingia Uturuki. Sakata la wanafunzi hao wa kike kutoka London kwenda kujiunga na wapiganaji wa Islamic State limekuwa limeshtua wengi.
Huku serikali ya Uturuki inasema ingechukua hatua kama ingepewa taarifa mapema Naibu Waziri Mkuu wa Bulent Arinc anatupa lawama moja kwa moja kwa Uingereza kwamba iliichelewa kuijulisha nchi hiyo kabla ya wanafunzi hao hawajaingia katika mji mkuu wa Instanbul.
"Tumefuatilia na tumezuia watu wapatao elfu kumi ambao hapo awali waliripotiwa kwetu kutaka kuingia Uturuki kwa tuhuma za kutaka kuendesha shughuli za kigaidi. Tumetimiza wajibu wetu. Kama Serikali ya Uingiereza ingetujulisha mapema maafisa wetu wa usalama wangechukua hatua madhubuti. Tunaamini kuna haja ya kuanganisha nguvu kwa pamoja ili kuratibu na kupambana na ugaidi." Alisema.
Wakati kukiwa na taarifa hizo za wanafunzi wa kike waliokuwa wakisoma London Uingereza kuingia nchini Syria kujiunga na Islamic State
Nayo serikali ya Ufaransa kwa mara ya kwanza imezikamata hati za kusafiria za raia wapatao sita ambao wanatuhumiwa kwenda nchini Syria kujiunga na wapiganaji hao wa Islamic State.
Waziri wa Mambo ya ndani wa ufaransa Benard Cazeneuve amesema kitengo cha ujasusi kinaamini kwamba watu hao walikuwa na mpango wa kusafiri na kwamba swala hilo linahusiana na mambo ya usalama.
"Tunaamini hatua hizi zilizochukuliwa zimefanikiwa kwa sababu kama raia wa Ufaransa watakwenda kupigana Iraq na Syria watasababisha hatari kubwa kwa usalama wa taifa wakati watakaporudi. Wanaweza kuendesha vitendo vya kigaidi kwa kiwango kikubwa." Alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni