Jumatano, 18 Februari 2015
TAARIFA RASMI YA MABADILIKO YA WAKUU WA WILAYA 2015.
TAARIFA RASMI YA
MABADILIKO YA WAKUU WA
WILAYA 2015
RAIS Jakaya Kikwete
amefanya mabadiliko ya Wakuu
wa Wilaya kwa kuwateua
Wakuu wapya 27,
kuwahamisha vituo vya kazi 64
na wengine 42 amewabakisha
kwenye vituo vyao vya kazi
vya zamani.
Akizungumza na waandishi wa
habari kwenye ukumbi wa
OWM TAMISEMI leo mchana
(Jumatano, Februari 18, 2015)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda
amesema mabadiliko hayo
yamesababishwa na kuwepo
kwa nafasi wazi 27 ambazo
zilitokana na wakuu wa wilaya
watatu kufariki dunia;
kupandishwa cheo wakuu wa
wilaya watano, kupangiwa
majukumu mengine wakuu wa
wilaya saba na kutenguliwa
kwa uteuzi wa wakuu wa
wilaya 12.
Hata hivyo, Waziri Mkuu
alisema, Rais Kikwete
amewabadilisha vituo vya kazi
wakuu wa wilaya 64 na
kuwabakiza kwenye vituo vyao
vya zamani wakuu wa wilaya
42.
Wakuu wa Wilaya wapya 27
walioteuliwa ni Mariam
Ramadhani Mtima anayeenda
Ruangwa; Dk. Jasmine B.
Tiisike anayeenda Mpwapwa;
Pololeti Mgema (Nachingwea);
Fadhili Nkurlu anayeenda
Misenyi; Felix Jackson Lyaniva
anayeenda Rorya na Fredrick
Wilfred Mwakalebela
anayeenda wilayaya
Wanging’ombe.
Wengine na vituo vyao kwenye
mabano ni Zainab Rajab
Mbussi (Rungwe); Francis K.
Mwonga (Bahi); Kanali
Kimiang’ombe Samwel Nzoka
(Kiteto), Husna Rajab Msangi
(Handeni), Emmanuel J. Uhaula
(Tandahimba); Mboni Mhita
(Mufindi); Hashim S. Mgandilwa
(Ngorongoro); Mariam M. Juma
(Lushoto); Thea Medard Ntara
(Kyela); Ahmad H. Nammohe
(Mbozi); Shaban Kissu
(Kondoa) na Stephen Zelothe
(Musoma).
Wengine ni Pili Moshi
(Kwimba); Mahmoud A.
Kambona (Simanjiro); Glorius
B. Luoga (Tarime); Zainab R.
Telack (Sengerema); Bernard
Nduta (Masasi); Zuhura
Mustafa Ally (Uyui); Paulo
Makonda (Kinondoni);
Mwajuma Nyiruka (Misungwi)
na na Maftah Ally Mohamed
(Serengeti).
Wakuu wa Wilaya saba ambao
uteuzi wao umetenguliwa lakini
watapangiwa kazi nyingine ni
Brig. Jenerali Cosmas
Kayombo aliyekuwa Simanjiro;
Kanali Ngemela E. Lubinga
(aliyekuwa Mlele); Juma S.
Madaha (aliyekuwa Ludewa);
Mercy E. Silla (aliyekuwa
Mkuranga); Ahmed R. Kipozi
(aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho
Gambo (aliyekuwa Korogwe)
na Elinas A. Pallangyo
(aliyekuwa Rombo).
Waziri Mkuu pia aliwataja
Wakuu wa Wilaya 12 ambao
uteuzi wao umetenguliwa
kutokana na sababu za umri,
kiafya na kuimarisha utendaji
Serikaini na wilaya zao kwenye
mabano kuwa ni James K. Ole
Millya (Longido); Elias Wawa
Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest
Msovella (Kongwa); Danhi
Beatus Makanga (Kasulu);
Fatma Losindilo Kimario
(Kisarawe); Elibariki E. Kingu
(Igunga); Dk. Leticia Moses
Warioba (Iringa); Evarista N.
Kalalu (Mufindi); Abihudi M.
Saideya (Momba); Martha J.
Umbulla (Kiteto); Khalid J.
Mandia (Babati) na Elias Goroi
(Rorya).
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATANO, FEBRUARI 18,
2015
‹ ›
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni