Ijumaa, 27 Februari 2015
MV DAR ES SALAAM YAANZA MAJARIBIO,YAENDA BAGAMOYO NA KURUDI DAR.
MV Dar es Salaam yaanza majaribio,
yaenda bagamoyo na kurudi Dar
Waziri wa Ujenzi Dk, John Magufuli leo
amewaongoza wananchi wa jiji la Dar es Salaam
kwenye majaribio ya uzinduzi wa Kivuko kipya
Cha MV DAR ES SALAAM kitakachofanya safari
zake kati ya Dsm na Bagamoyo.
Mamia ya wananchi wakiwa na furaha ya usafiri
huo wamesafiri pamoja na Waziri Dk Magufuli
bure kutoka jijini Dar hadi Bagamoyo kwenda
na kurudi kujionea huduma hiyo itakayoanza
kutolewa siku za usoni.
Akizungumza kwenye majaribio hayo Waziri Dk
Magufuli amesema lengo la Serikali kufanya
hivyo ni kutaka kuharakisha maendeleo ya
wananchi kwa njia yeyote akiongeza kuwa
usafiri wenye tija unaongeza pato la taifa.
Amesema Kivuko hicho kitazinduliwa rasmi hivi
karibuni na kuanza safari zake mara moja,
hivyo wasafiri wanaokwenda bagamoyo
hawatalazimika tena kutumia barabara.
"Mbali na kuongeza pato la taifa pia kivuko hiki
kitapunguza kwa namna moja ama nyingine
foleni za jiji la Dar es Salaam, amsema Magufuli.
Amesema Serikali itaendelea kubuni mbinu
mbalimbali za kimaendeleo ili watanzania
waweze kufaidika na kujikomboa kimaisha.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni