Jumanne, 10 Februari 2015

MIDO YENYE NDOTO YA KUCHEZA SOKA NJE YA NCHI.

Alex Mayele wa tano kutoka kushoto akiwa ndani ya kikosi cha timu ya MASHUJAA FC iliyoko wilayani Nachingwea amejiwekea malengo ya kutimiza ndoto yake ya kuwa na maisha ya soka nje ya nchi.

DARAJA LA KUMVUSHA NJE KISOKA.

Mchezaji Alex amefunguka zaidi na kuweka wazi timu ambayo anadhania itamfikisha kule anakofikiria,kuwa ni SIMBA SC wekundu wa Mslmbazi.

SABABU ZA KUCHAGUA SIMBA KAMA DARAJA.

Alex ametiririka zaidi na kusema kwamba "naipenda simba tangu nikiwa mtoto mpaka hivi sasa na pia Simba ni timu ambayo haina hiyana punde mchezaji anapopata timu nje ya nchi."

MCHEZAJI ANAYEMVUTIA.

Hakusita kumtaja mchezaji anayemvutia kwa sasa nchini kuwa ni Jonas Mkude mido mahiri nchini anayekipiga ndani ya wekundu wa Msimbazi.Anapenda kuona mkude akiwa ndani ya mido dakika zote tisini za mchezo.

MATUMAINI.

Kutokana na mazoezi ambayo anaendelea kuyafanyia kazi na kurekebisha pale anapoona amekosea,mchezaji Alex ana matumaini makubwa ya kufika kule anakokusudia kufika katika maisha yake ya soka.Nasi kama wadau wa soka tungependa kuona au kusikia amefika safari yake.MUNGU MBARIKI ALEX,MUNGU LIBARIKI SOKA LA TANZANIA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni