Jumatatu, 23 Februari 2015

JB: Rais Kikwete Tutakufa Maskini


Mwigizaji nguli na muongozaji wa filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’, amesema kuwa pamoja na kuendelea kulia juu ya kuibiwa kazi zao, anamkumbusha Rais Jakaya Kikwete kutimiza ahadi yake aliyowahi kusema kwenye msiba wa nguli wa filamu, Steven Kanumba kuwa atawashungulikia wale wote wanaoiba kazi za wasanii na kutoa kopi.
 
JB alitoa ombi  kwa uchungu ambapo alifunguka kuwa pamoja na kuwepo kwa wasambazaji lakini bado wasanii wamekuwa wakilia kila siku hasa pale wanapopeleka filamu zao sokoni.
 

“Rais wetu alitoa kauli kuwa atawashughulikia wale wote wanaohusika na wizi wa kazi zetu, lakini hadi leo bado hajatekeleza hilo, lakini hatuwezi kushindwa kusema kuwa tunaumia sana, tunaomba atusaidie  maana  tunakufa  masikini” alisema JB.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni