Jumatatu, 16 Februari 2015

WANYAMA WAFUKUZISHA KAZI WATU AUSTRALIA.

Mbwa wanaopewa mafunzo

Watu 10 wafukuzwa kazi kwa kosa la kutumia wanyama hai, kutoa mafunzo. Wakuu wa mbio za mbwa Nchini Australia, wamewafukuza kazi zaidi ya watu 10 kutoka katika sekta hiyo, kwa kosa la kutumia wanyama hai kuwapa mafunzo mbwa wao, wanaoshiriki mbio hizo. Picha za video zilizopigwa kisiri, zilionyesha watoto wa nguruwe, sungura na panya buku, wanatumika kuwapa mafunzo ya kuwinda mbwa hao. Wanaonekana wakikimbizwa na kuliwa wangali hai.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni