Mrembo na mwigizaji wa filamu za kibongo, Aunt ezekiel amejikuta
akitoa maneno makali baada ya mashabiki wake kumshabulia kwa maneno
baada ya kuweka mtandaoni picha ikimuonyesha amevalia kinguo ambacho kwa
maoni ya mashabiki hao hakistahili kuvaliwa na mwanamke mjamzito na
kibaya zaidi alionekana mkononi ameshika chupa ambapo wengi waliiona kama
niyakilevi.
Aunty Ezekiel alibandika picha hiyo hapo juu akiwa na jamaa kwenye ukurasa wake mtandaoni na kuandika maneno “My best friend,my love,my kimoko I love him so much”
Baada ya kubandika ujumbe huo baadhi ya mashabiki wake walionyeshwa
kukerwa na mavazi na sehemu alikokuwepo nakumtaka atulie nyumbani alee
mimba yake kwani kwasasa inaonekana kuwa na ya zaidi ya miezi nane na
wiki kadhaa.
“Ungetulia tu nyumbani ukasubiri kujifungua salama,mjamzito
kuzurura namna hiyo na mijanaume sio poa kabisa tena na kilaji mkononi
harafu pia hata hayo mavazi mmmh!!” alisema mmoja wa shabiki na kuungwa mkono na wengine wengi.
Baada ya muda kidogo aunty ezekel akaibuka na kuandika ; “Plz
msiwe bac mnaongea kitu kabla ujajua undani wake, ni vizuri kuuliza
kuliko kuandika tu ilimradi na wewe uonekane umeongea hiyo nguo ni
special kwa mama mjamzito na hapo juu inampira wakutosha tu na mapajani
ndio inabana sasa”
Lakini majibu hayo yalionekana kuamsha maneno zaidi ya kumponda Aunty
ambae nae mwishoni alionekana kushindwa kuvumilia na kutoa matusi mazito ambayo sio busara kuyabandika hapa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni