Alhamisi, 26 Februari 2015
WAKRISTO ZAIDI WATEKWA NYARA SYRIA.
Wakristo zaidi watekwa nyara Syria
Kuna hofu kuwa raia wakristo kutoka Syria
wametekwa nyara na wanamgambo wa Islamic
State.
Duru kutoka kwa jamii hiyo sasa inathibitisha
kwamba zaidi ya raia 200 walitekwa nyara
Jumanne baada ya vijiji kadhaa kushambuliwa
kazkazini mwa Syria.
Wengi wa waliotekwa nyara ni wanawake na
wazee.
Wakati huo huo, mapigano yangali yakiendelea
katika maeneo yaliyoko karibu na mji wa Hassaka.
Kuna taarifa zinazosema kuwa makanisa
yameteketezwa moto na kundi la IS katika vita
hivyo vikali kati ya wanamgambo hao na makabila
ya Wakurdi wanaoungwa mkono na wakristo wenye
silaha.
Taswira kamili ya mkasa uliowakumba wakristu
hawa wa Syria ndio mwanzo unaanza kujitokeza.
Wakristo kutoka Syria wameanza kutoroka
wanakoishi
Lakini kikundi cha wapiganaji wa kikristu kimetoa
madai kuwa idadi hiyo ni kubwa hata zaidi ya hiyo.
Kimedokeza kuwa zaidi ya watu mia tatu hamsini
wametekwa.
Huku hayo yakiarifiwa waumii wengine wa kikristu
wameanza kukimbia avijiji vyao wakihofia
kushambuliwa na wanamgambo wa Islamic State.
Na bado vita vinaendelea huku waislamu hao
wakikabiliana na waasi wa kikurdi pamoja na
washirika wao wa kiksristu katika mji wa Hassaka.
BBC.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni