Jumapili, 15 Februari 2015

RUNINGA ZILIZOJIZIMA KENYA KUPIGWA FAINI.

Mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya sasa inasema kuwa itavipiga faini vituo vya uninga vya NTV,KTN,Citizen na QTV nchini Kenya kwa kuzima matangazo yao kufuatia hatua ya serikali kuhamia katika matangazo ya dijitali. Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Francis wanguzi amewaambia wana habari kwamba hatua zitachukuliwa dhidi ya runinga hizo kwa kukiuka sheria. ''Lazima waadhibiwe'',alisema wanguzi baada ya runinga hizo kufunga matangazo na hivyobasi kuwanyima wakenya fursa ya kuona taarifa zao katika vituo vya DSTV,Zuku na vituo vyengine vya kurusha matangazo. Mda mfupi baada ya vituo hivyo kuzimwa siku ya jumamosi,DSTV iliweka taarifa katika mtandao wa twitter ikiwataka wakenya wanaohitaji kuangailia habari kujaribu kufanya hivyo kupitia vituo vyengine vya runinga. Vituo vivyo viliendelea kufunga matangazo yao siku ya jumapili baada ya maafisa wa mamlaka hiyo ya mawasiliano kufunga mitambo yao ya kurusha matangazo hewani katika eneo la Limuru.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni