Jumatano, 11 Februari 2015

MAPENZI NI ZAWADI YA PEKEE AMBAYO HUWEZI KUPATA KWA KILA MTU.

Unasema wa nini wapo wanaojiuliza watampata lini, msidharauliane Dharau ni tabia chafu ambayo imekuwa ni ya kawaida miongoni mwa wale ambao wana wenza wao. Dharau ni tabia chafu ambayo imekuwa ni ya kawaida miongoni mwa wale ambao wana wenza. Kuna watu wanaume kwa wanawake wamekuwa na maneno na matendo machafu kwa wenza wao, kwa bahati mbaya zaidi ni kwamba hata wanapoombwa kuacha tabia hizo, huwa na maneno ya kukera zaidi. Wengine wanadharauliana kwa sababu labda anajiona yeye ni bora zaidi, anajiona ana fedha zaidi, anajiona maarufu zaidi na kadhalika. Anashindwa kuelewa kwamba hata kama labda ni kweli akawa ana ubora zaidi, lakini hata vichaa hutiwa mimba, hata wenye ubaya wa kila aina wana watu wao wanaoweza kula nao sahani moja katika suala la uhusiano. Hata wenye sura mbaya, kuna watu wanawataka. Acha kuringa kwa sababu zozote zile, unapokuwa na mwenzi, jambo la msingi ni kuheshimiana kwa sababu kuwa na wewe haina maana kwamba ni kweli kuwa hakuna mwingine anaweza kuwa nao au kuwa naye. Ndege kuacha mti huu kwenda kutua mti mwingine haina maana kwamba mingi aliyoacha kuitua inanuka kinyesi au inawaka moto, bali ni hali ya kawaida katika maisha, kwamba huwezi kutua kwenye miti yote, si ndiyo jamani. Ndege kuacha miti hii kwenda kutua ile haina maana kwamba miti hii iliyoachwa ni mibaya. Ilivyo ni kwamba inawezekana kabisa kwamba huenda baadhi ya miti ambayo ndege huyo aliacha kuitua ina uzuri wake, isipokuwa pengine ni kwa sababu ya akili mbaya na huyu ndege akaamua kwenda kutua kwenye ile mingine. Ukweli ni kwamba watu wanaingia kwenye uhusiano siyo kwa lengo la kutafuta watu wa kuwatukana matusi; wengi wanaingia kwenye ndoa wakiwa na imani kwamba watapata furaha, lakini kwa sababu mbalimbali, wengine wamekuwa wakijikuta wanaingia kwenye shida mwanzo mwisho. Mtu anapoishi kwenye uhusiano ambao haumpi amani, huweza kuamua chochote hata kama ni kibaya, hata hivyo ukweli ni kwamba ni suala la msingi kwa watu kuelewa kwamba matatizo katika maisha yapo. Wengine wamekuwa wakisema aaah mwenza wangu namfanyia mazuri, lakini hajali…ndugu yangu ni kweli inawezekana unafikiri unafanya mazuri, yasiwe mazuri. Ndio maana nikaona ni vizuri kuandika mada hii ili kusaidia kufahamu kwamba yapi kweli ni mazuri katika suala zima la mapenzi; A.MAPOKEZI MAZURI: Ni kwamba baada ya mumeo kurejea kutoka kazini, safarini, au kokote, jitahidi kumpokea kati hali nzuri kwa maana kwamba onyesha sura ya uchangamfu, lakini zaidi ya yote hakikisha unakuwa mwenye kuvutia kuanzia mavazi na mwili wako kwa ujumla hasa unatakiwa kuoga na kutumia manukato mazuri. *Unapokutana na mumeo kwa mara ya kwanza akitokea katika mihangaiko ya miasha au safarini, anza kwanza na habari nzuri…baada ya muda akiwa ametulia ndipo uanze kumwambia habari mbaya.Maana kuna wengine utasikia wanawapokea waume zao kwa habari mbaya “Mfanyakazi wa ndani leo amenikwaza sana, nimemtuma maji kaniambia kachoka…kanikwaza sana natamani atoke”. Ndugu yangu ni hekima kuangalia maneno gani ya kuanza nayo…matatizo yapo, kwa maana hiyo unapaswa kuyafahamu na kuchukua hatua za maana. Ni vizuri kumpokea mumeo kwa maneno yaliyojaa upendo, mapenzi na shauku ya kuwa pamoja nae. Lakini pia ni suala la msingi kwa mwanaume kuhakikisha hawi na tatizo la nguvu za kiume, mara kadhaa nimekuwa nikilizungumzia suala hili na tiba zake, lakini kuna wanaume wengi hawaoni umuhimu wa kuchukua tahadhari, wanafanya mizaha…siyo kweli wanawake wanashindwa kujinunulia nguo, magari nk…hakikisha mwanaume unakuwa imara, amini ninachokwambia utasaidiwa siku moja.Atavumilia atachoka. MAMBO MENGINE YA MSINGI: *Penda kuuchunguza mwili mwako ili kuona kama ugonjwa wowote au la. Ni jambo linalokwaza, kuna wengine utashangaa kwamba mchana mzima hakusema kwamba anaumwa, lakini unapomwambia nahitaji hiki, ndipo naye anaanza kulalamikia aaah kichwa kinauma, aaah kiuno nk. *Katika suala zima la maisha ya wanandoa, ni muhimu kupenda kuvaa nguo za kuvutia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni