Jumanne, 24 Februari 2015

Machafuko Ukraine yatazusha vita:Putin

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema machafuko Mashariki mwa Ukraine yanaleta wasiwasi wa kuweza kuzuka kwa vita na mwendelezo wa mzozo.

Akizungumza kupitia televisheni Putin amesisitiza kuzingatiwa kwa mpango wa Amani ya mashariki mwa Ukraine uliojadiliwa Minsk na kupitishwa na baraza la usalama la umoja wa mataifa

Hata hivyo kwa mara nyingine Rais Putin amekanusha madai ya majeshi yake kushiriki katika mzozo.

Kiongozi huyo pia ameyaraja mataifa ya Urusi, ujerumani na Ufaransa kuma washirka mhimu katika utatuzi wa mgogoro huo na kwamba kupitia makubaliano ya Minsk pekee ndiyo itakuwa njia pekee ya kurejesha Amani ya Ukraine.

Kuhusiana na kutuhumiwa kwa taifa lake kuhusika katika mzozo huo Putin amesema wakati mwingine anashtushwa na kauli zinazotolewa na viongozi wa Ukraine dhidi ya Urusi,mfano tuhuma kuwa mamlaka za Urusi zilihusika na machafuko ya viunga vya Maidan mwaka mmoja uliopita.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni