Ijumaa, 27 Februari 2015
BENSOUDA AWASILI UGANDA,KUNANI?
Bensouda awasili Uganda,kunani?
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya
kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC Fatou
Bensouda amewasili nchini Uganda ili kutafuta
ushahidi kuhusu kesi ya aliyekuwa kamanda mkuu
wa wapiganaji wa LRA nchini Uganda .
Dominic Ongwen ambaye alisema alitekwanyara na
LRA akiwa mtoto alifikishwa mbele ya mahakama
ya ICC mjini Hague mnamo mwezi Januari
akikabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita.
Mwandishi wa BBC mjini Kamapala anasema kuwa
Bensouda atazuru kazkazini mwa Uganda katika
ziara ya siku tano ili kuzungumza na mashahidi
mbali na kutembelea maeneo yaliotekelezewa
uhalifu huo.
Pia anatarajiwa kukutana na rais Yoweri Museveni
wa Uganda ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa
wa mahakama hiyo ya ICC akiishtumu kwa
kuwabagua viongozi wa Afrika.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni