Jumanne, 24 Februari 2015
Nyaraka za siri zamuumbua,Netanyahu
Nyaraka za siri zilizochapishwa na gazeti la Guardian la London ambazo
waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alizihusisha na mpango wa
nyuklia wa Iran 2012 imebainika kuwa madai hayo hayakuungwa mkono na
idara za usalama za Israel. Tuhuma hizo za Israel dhidi ya Iran
zilitolewa na Netanyahu mwaka 2012. Moja ya taarifa hizo zilizovuja
kupitia jalada hilo la Mossad lilionyesha kuwa Iran haikuwa na mpango wa
uzalishaji Uranium kwa matumizi ya kawaida bali kutengenezea mabomu.
Afisa mwandamizi wa Irael ameeleza kuwa jalada hilo la Mossad lililobeba
kashfa hiyo kamwe halihusiani na kubeza madai ya Waziri mkuu wa Israel
Benjamin Netanyahu kuhusia na Iran na mpango wake wa Nyuklia. Chapisho
hilo linadaiwa kuwa ni moja kati ya mamia ya machapisho ya siri
yanayobeba taarifa za uchunguzi zilizofanywa na Al Jazeera kwa
kushirikiana na gazeti la Guardian.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni