Jumanne, 17 Februari 2015
MAAFISA POLISI 20 WAUAWA AFGHANISTAN.
Maafisa Polisi 20 wauawa Afghanistan
Wanamgambo wa Taliban wamekuwa
wakihatarisha usalama wa Afghanistan
Maafisa Mashariki mwa Afghanistan wamesema
maafisa wa Polisi 20 wameuawa katika
mashambulio kadhaa.Watu wanne wameripotiwa
kuvalia mavazi ya Polisi na kuingia katika Ofisi za
makao makuu ya Polisi katika jimbo la Logar, na
kujilipua.
Gavana wa Jimbo hilo Niaz Muhammad Amiri
ameiambia BBC kuwa Maafisa wengine wanane
walijeruhiwa.Wengi kati ya waliopoteza maisha
walikuwa wakipata chakuwa wakati wa
mapumziko.
Kumekuwa na ongezeko la mashambulizi ya
Wanamgambo miezi ya hivi karibuni wakati ambapo
vikosi vya usalama vikiwa vimechukua udhibiti wa
nchi hiyo kutoka kwa Majeshi ya NATO.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni