Usiku wa kuamkia leo mamilioni ya
watu kote duniani wamekuwa wakijadiliana kwa kina kuhusiana na rangi ya
rinda moja lenye rangi mbili.
Aliyezua mjadala huo aliipiga picha
rinda la mwanamke akilalama kuwa ''ee bwana nyie mnisaidie mimi na
familia yangu tumeshindwa kuafikiana kuhusu rangi ya rinda hili''''je ni la Dhahabu na Nyeupe ama ni leusi na samawati ''bluu''
Na kila aliyejaribu kuijibu alizidisha utata.
Mwanamziki Taylor Swift akapalia moto aliposema kuwa rinda hilo ni leusi na samawati(bluu)
“baada ya kutafiti rangi tofauti chuoni kwa miongo mitatu mwanachuoni Jay Neitz, wa chuo kikuu cha Washington kilichoko Seattle, marekani amesema utata huu unatokana na tofauti za genetiki.
Watu wenye umri mkubwa wanaupungufu wa uwezo wa kuona rangi ya samawati(bluu) kwa hivyo watasema kuwa rinda hilo ni leupe na dhahabu lakini kimsingi ni ulemavu wa macho , alisema Neitz.
Mwanachuoni huyo hata hivyo alitamatisha maoni yake kwa kusema kuwa rangi haswa ya rinda hilo inamtegemea saikolojia ya yule anayeitazama.
Kazi kwako msomaji je ni ya rangi gani rinda hili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni