Jumatatu, 23 Februari 2015

Johari Atubu Kumpora Ray kwa Mainda

Mrembo na mwigizaji  wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ amekiri kwamba wakati anaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na nyota wa fani hiyo, Vincent Kigosi ‘Ray’ alijua yupo na nguli wa filamu, Ruth Suka ‘Mainda’.
 
Johari alikili hayo Katika mahojiano mafupi na Gazeti moja la udaku siku ya Jumanne ya wiki iliyopita  jijin Dar, mahojiona yalikuwa hivi.
 
Mwandishi: “Kwanza napenda kujua kama kweli umerudiana na Ray maana kuna minong’ono kwamba penzi lenu kama zamani.”
Johari: “Siyo kweli. Kwanza mimi sipendagi hayo maswali miaka yote mambo ni hayohayo, sasa nimekua mtu mzima na mambo lazima yabadilike.”
 
Mwandishi: “Kwa hiyo huna uhusiano na Ray?”
Johari: “Sina.”
 
Mwandishi: “Sasa kama ni kweli mbona ofisi yako bado ipo nyumbani kwa akina Ray? (Sinza-Mori).”
Johari: “Kazi zinakwenda kama kawaida. Mimi na Ray kwenye kazi hatuna tatizo lolote, asubuhi nafungua ofisi baadaye watu wanakwenda ‘lokesheni’.”
 
Mwandishi: “Hebu niambie kuhusu Mainda. Wakati unaingia kwenye uhusiano na Ray ulijua kuna Mainda?”
Johari: “Ndiyo nilijua.”
 
Mwandishi: “Ikawaje ukaingia sasa?”
Johari: “Hilo swali silitaki.”
 
Mwandishi: “Oke, je wewe na Mainda mna mawasiliano mazuri?”
Johari: “Yes! Ikibidi kuwasiliana tunawasiliana, tuko sawasawa.”
 
Mwandishi: “Inasemekana umefunga pub yako ya kuuza pombe, ni kweli?”
Johari: “Ilibidi nifunge, mwenye nyumba alisema hapendi niuze pombe pale, natafuta sehemu nyingine.”
 
Mwandishi: “Nashukuru sana Johari.”
Johari: “Poapoa.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni