Polisi nchini Tanzania wamesema wanawasaka watuhumiwa waliowajeruhi askari sita kwa risasi mkoani Tanga. Askari hao walijeruhiwa wakati wakifanya kazi ya kuwatafuta watuhumiwa wa uhalifu wa kutumia silaha wanaodaiwa kuwa walijificha eneo moja nje ya mji wa Tanga wakiwa na silaha. Awali kulizagaa taarifa na hofu kuwa wahusika walikuwa na itikadi za kigaidi, lakini taarifa ya maandishi iliyotolewa na polisi imewaita watu hao kuwa ni majambazi na kwamba msako wa kuwatafuta unaendelea. Hata hivyo taarifa haikuleleza wanaotafutwa ni watu wangapi, ingawa imetaja kuhusika kwa jeshi lenye silaha jambo linaloashiria mapambano yalikuwa makali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni