Jumatano, 25 Februari 2015
WAFUASI WATATU WA IS,WAKAMATWA MAREKANI.
Maafisa wa Polisi nchini Marekani,wamewakamata
wanaume watatu kwa njama za kuwaunga mkono
wanamgambo wa dola ya kiislam Islamic State.
Wanaume wote hao ni wakaazi wa mji mkuu wa
nchi hiyo New York. Wawili kati yao wanatokea
Kazakhstan na Uzbekistan, na mwingine ni wa
kutoka Uzbek yeye alimakatwa mjini Florida.
Wawili kati ya wanaume hao walikuwa na mpango
wa kusafiri kuelekea nchini Syria
Kwa mujibu wa Shirika la Ujasusi la Marekani FBI
watuhumiwa wawili kati yao walitishia kuwaua
maafisa wa polisi kama wasingeweza kusafiri
kwenda Syria.
Hata hivyo mtuhumiwa mmoja kati ya watuhumiwa
hao alikuwa na mpango wa kumuua rais Marekani
Barack Obama,wamesema FBI.
Kamishina wa polisi mjini New York , William
Bratton anasema maneno yao ndiyo
yanayodhihirisha nia yao.Hata hivyo inadaiwa kuwa
ni dhahiri kutokana na matamshi yao walikuwa na
mpango wa kusafiri hadi nchini Syria, baada ya
kukamilisha malengo yao ya kijipatia silaha ambazo
wangezitumia kuwashambulia maofisa wa polisi.
Bratton amesema ilikuwa ni mpango wao wa wazi
kwamba hawakuhitaji kwenda,huku malengo yao
ikiwa ni kujipatia silaha kama vile bunduki aina ya
mashine gani, kwa lengo la mashambulizi maalum
dhidi ya maofisa wa polisi ambapo maneno yao ya
kuhamasishana yalikuwa wazi kwa mjibu wa
maneno yao.
Nje ya mahakama mjini New York walikofikishwa
washitakiwa wawili mwanasheria wa washitakiwa
hao, Adam Parumata ameelezea kutoridhirishwa na
mwenendo wa mashitaka hayo dhidi ya wateja
wake.
"Kama tuhuma hizi ni za kweli,na bado ni tuhuma
tu, zinatufanya kujiuliza maswali mengi kwa jinsi
serikali inavyowachukulia vijana hawa,na watu wa
dini ya Kiislam ndani ya Marekani. Kwani wapo
katika uangalizi mkali na wa aina yake,hakuna
ruksa kujibu,kuzungumza, kudadisi wala
kueleweshwa. Kinachofanyika ni mbio mbioni
kuwafungulia mashtaka, kuwaweka kizuizini.
Nataka kusisitiza jambo kwa kila mtu leo kuwa haki
ya mshitakiwa ni kwamjibu wa sheria za
Marekani,hivyo tunafanya kila linalowezekana
kupigania haki katika kesi hii kwa lengo la kulinda
haki”amesema Parumata.
BBC.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni